Tanzania na JICA kushirikiana katika kujenga uwezo matumizi bora ya gesi asilia

Tanzania na JICA kushirikiana katika kujenga uwezo matumizi bora ya gesi asilia

chuchu2020

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
5
Reaction score
2
TANZANIA NA JICA KUSHIRIKIANA KATIKA KUJENGA UWEZO MATUMIZI BORA YA GESI ASILIA

Wizara ya Nishati pamoja Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) wamesaini makubaliano ya kutekeleza mradi wa kujengea uwezo Wataalam wa Wizara na Taasisi zake katika eneo la kuendeleza matumizi bora ya Gesi Asilia ili kuiwezesha Tanzania kuendelea kunufaika kiuchumi na rasilimali hiyo.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania, ARA Hitoshi tarehe 16 Mei, 2023 jijini Dar es Salaam.

Makubaliano hayo yatapelekea wataalam wa Tanzania kuongeza ufanisi katika kufanya mipango na kutekeleza miradi ya matumizi ya Gesi Asilia kwa kuzingatia pia suala la utunzaji wa mazingira.
 
Back
Top Bottom