SoC04 Tanzania na kanda zake kimaendeleo

SoC04 Tanzania na kanda zake kimaendeleo

Tanzania Tuitakayo competition threads

nottorious kadege

New Member
Joined
May 29, 2017
Posts
1
Reaction score
1
MUAROBAINI WA MAENDELEO YETU NI NISHATI.

Tanzania tume pata uhuru wetu mwaka 1961 na katika kipindi hicho ni mikoa miwili tu ilio kuwa na umeme wa uhakika mbayo ni Tanga na Dar Es Salaam. Tanga kwa sababu kulikuwa na viwanda vya mkonge na Dar es Salaam kwa sababu kulikuwa na uhitaji katika uendeshaji wa stesheni ya umeme.

Sasa hivi ni miaka 62 ya uhuru lakini bado tuna pambana na umeme mdogo wa mahitaji ya nyumbani na kidogo kwa viwanda vidogo hasa kwa uchenjuaji wa nafaka.

Kama nchi tumejenga bwawa la Mwalimu Nyerere ili kutatua tatizo la umeme na nishati kwa ujumla je tutaweza kufikiwa lengo la kuitoa nchi yetu kutoka nchi ya umasikini wa kati hadi kuwa nchi ilio endeleo?. Jibu ni hapana sasa illi kutoka hapa tulipo tufanyaje kama nchi.

Kuzalisha umeme kwa ukanda kwa kadili itavyo wezekana, mfano mikoa ya nyanda za juu kusini itumie makaa ya mawe kuzalisha umeme wao ambayo tumeambiwa yako maelfu ya tani huko kiwila mkoni mbeya, lakini pia mikoa ya kanda ya kati wanaweza kuzalisha umeme kwa njia ya upepo ambao eneo hilo kuna tafiti zilifanyika na kugundulika kuwa inawezekana.

Kanda ya Pwani wanaweza kutumia umeme wa mawimbi ama umeme wa gesi asilia ambayo tayari imefika Dar es Salaam kutoka Mtwara, umeme wa jua na umeme wa nguvu au joto la dunia (geothermal energy) pia huweza kutumika maeneo ya rukwa ambako visima vya maji mito vipo vingi.

Nishati ikizalishwa katika eneo husika inaweza kupunguza gharama za usafirishaji wa umeme wenyewe na gharama za watumiaji kwa kiwango kikubwa mno.

Lakini nashauri Tanesco isiwe nchi nzima kama tasisi moja ila iwe ngazi ya kanda au mikoa lakini ziwe chini ya wizara kama zilivyo malka za maji katika mikoa au halmashauri hii itapunguza urasimu na mnyororo mrefu wa amri (chain of command) katika kufanya maamuzi.

Matumizi ya madini ya urari (uranium)katika kuzalisha umeme, Tanzania ni moja ya nchi chache ambazo kumegundulika madini ya urari ambayo vumeme mkubwa unao hitajika katika viwanda vikubwa vya kuzalisha magari na kufua vyuma huweza kuzalishwa kwenye vinu hivi kama nchi tuna weza kuwa na mpango mkakati wa kuwa na kinu cha madini ya urari ndani ya miaka kumi hadi kumi na tano

Tukiwa na umeme wa uhakika ulio na gharama nafuu Sana ni rahisi kuvutia wawekezaji wakubwa wa magari au vipuri vya mgari na mitambo mbalimbali kwa sababu malighafi tunazo mfano tuna maelfu ya tani ya madini ya chuma huko mchuchuma na liganga.

Nishati ya umeme iendane na upanuzi wa nishati ya gesi asilia katika matumizi kwa sababu zaidi ya watanzania asilimia 80 wanatumia mkaa na kuni kitu ambacho sio rafiki kwa mazingira na afya
 
Upvote 3
Back
Top Bottom