Tanzania na Kenya tumeweka ruzuku kwenye mafuta. Rais Museveni asema hiyo haisaidii yeye ataka Magari ya Umeme

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wakati Tanzania tunapata unafuu wa Bei za mafuta kupitia ruzuku lakini Rais Museveni wa Uganda amesema ruzuku haisaidii lolote.

Uganda wameanza Mfumo wa kuyabadili magari yaanze kutumia Umeme.

Rais Museveni alikuwa akichangia nada kwenye kikao cha wakuu wa nchi za EA.

Chanzo: ITV Habari
 
Wakati Tanzania tunapata unafuu wa Bei za mafuta kupitia ruzuku lakini Rais Museveni wa Uganda amesema ruzuku haisaidii lolote

Uganda wameanza Mfumo wa kuyabadili magari yaanze kutumia Umeme

Rais Museveni alikuwa akichangia nada kwenye kikao cha wakuu wa nchi za EA

Chanzo: ITV habari
Huyu mzee ana mambo ya hovyo sana....suala la magari ya umeme sio leo..
Kwa wakati huu ambapo ndio kuna songombingo ni hatua gani anachukua?
 
Hivi Uganda si wanachimba mafuta?
Hadi wanajenga bomba kuuza nje mafuta kupitia Tanga,
Imekuwaje tena? Afrika tuna safari ndefu sana, tukifika tumechoka sana,
Hawajaanza kuchimba ndiyo maana bomba la mafuta halijalazwa kwenye eneo la Tanzania
 
Kama akili iliochoka inawaza kwa ufanisi hivyo nafikiri hio akili inatufaa zaidi kuliko akili ambayo inawaza kutoa billion 1OO kama suluhu ya kupanda kwa bei ya wese.
Uwezo WA kuagiza magari ya umeme si mchezo bei yake hata hivyo vituo vya kuchaji magari sidhani kama Huko Uganda vinazidi 5.
Ongezeko la bei ya mafuta ni changamoto inayohitaji utatuzi wa haraka tofauti na kusubiri magari ya umeme ambayo Kwa huku Africa tutachukua miaka 10 mbele
 
Mbona 7 7 magari ya Umeme yameuzwa kwa fujo!
 
Wanasiasa ni wajanja sana! Museven anaweza kusema hivyo ili kuwapumbaza wananchi wanaotaka nafuu ya bei huku akiwa hataki kutenga fedha kwa ajili ya ruzuku ya mafuta.

Actually kabla ya ruzuku(Subsidy) kuna kodi mwambie aondoe/apunguze kodi kwenye mafuta kama atakubali.
Hata hivyo Kinachofanyika Tanzania na Kenya ni janjajanja tu kuweka fungu dogo la ruzuku baada ya kuvuna mapesa mengi kupitia kodi ya mafuta kiasi cha bei kutokua himilivu.

Yeye mwamba Museven karuka huo msala jumla kwa kuhamishia mada kuzunguzia habari ya magari ya umeme huku akijua hayaji leo wala kesho. Ulaya kwenyewe walikoazisha hii agenda ya magari ya umeme bado asilimia kubwa mno wanatumia magari ya mafuta.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Wakati Tanzania tunapata unafuu wa Bei za mafuta kupitia ruzuku lakini Rais Museveni wa Uganda amesema ruzuku haisaidii lolote.

Uganda wameanza Mfumo wa kuyabadili magari yaanze kutumia Umeme.

Rais Museveni alikuwa akichangia nada kwenye kikao cha wakuu wa nchi za EA.

Chanzo: ITV Habari
Nilishawaambia watu tangu kitambo sana kuwa mradi wa bomba la mafuta hautafanyika kamwe kutokana na sababu nyingi. Sasa naona hata Museveni mwenyewe ameshaona hilo.
 
Uwezo WA kuagiza magari ya umeme si mchezo bei yake hata hivyo vituo vya kuchaji magari sidhani kama Huko Uganda vinazidi 5.
Ongezeko la bei ya mafuta ni changamoto inayohitaji utatuzi wa haraka tofauti na kusubiri magari ya umeme ambayo Kwa huku Africa tutachukua miaka 10 mbele
Ziko gari za nusu umeme nusu mafuta ama Hybrids. Nadhani ndio zinaweza kuwa mkombozi kwa kipindi hiki kigumu. Mfano mzuri ni Toyota Prius. Hio gari haina bei ya kutisha kiasi hicho.
 
Kama akili iliochoka inawaza kwa ufanisi hivyo nafikiri hio akili inatufaa zaidi kuliko akili ambayo inawaza kutoa billion 1OO kama suluhu ya kupanda kwa bei ya wese.
Hawa Uganda,si wameanza kuvhimba mafuta?Ambayo yatasafirishwa lwa bomba la mafuta hadi bandari ya Tanga au Ugsnda wamesahau
Wakati Tanzania tunapata unafuu wa Bei za mafuta kupitia ruzuku lakini Rais Museveni wa Uganda amesema ruzuku haisaidii lolote.

Uganda wameanza Mfumo wa kuyabadili magari yaanze kutumia Umeme.

Rais Museveni alikuwa akichangia nada kwenye kikao cha wakuu wa nchi za EA.

Chanzo: ITV Habari
Uganda si wameanza kuchimba mafuta?Na kusafirisha hadi bandari ya Tanga?Au wamesahau?
 
Kama akili iliochoka inawaza kwa ufanisi hivyo nafikiri hio akili inatufaa zaidi kuliko akili ambayo inawaza kutoa billion 1OO kama suluhu ya kupanda kwa bei ya wese.
Hawa Uganda kweli akili imechoka,wao si wameanza kuchimba mafuta,na kusafirisha nje,kupitia bandari ya Tanga,iweje watafute gari za umeme,wakati mafuta wanachimba wenyewe.
 
Ziko gari za nusu umeme nusu mafuta ama Hybrids. Nadhani ndio zinaweza kuwa mkombozi kwa kipindi hiki kigumu. Mfano mzuri ni Toyota Prius. Hio gari haina bei ya kutisha kiasi hicho.
Toyota Prius ya aina hiyo bei yake ni shilingi milioni sitini hiyo sio bei ya kutisha?
 
Back
Top Bottom