SoC04 Tanzania na kilio cha mtandao

SoC04 Tanzania na kilio cha mtandao

Tanzania Tuitakayo competition threads

silinu

New Member
Joined
May 10, 2024
Posts
3
Reaction score
0
Tanzania ni jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Muunganiko huu uliofanyika 26,April,1964 takeibani miaka 60 sasa ndo ulizaa Tanzania.

Tatizo la mtandao(network)
Tangu uhuru,Tanzania na Nchi nyingine Afrika na duniani Kwa ujumla zimekuwa zikifanya jitihada za makusudi Ili kuendana na teknolojia ya ulimwengu.
Licha la serikali ya Tanzania kufanya juhudi mbalimbali katika kutatua changamoto za kutokuwepo Kwa mtandao katika badhi ya maeneo,suala ya mtandao(network) Bado ni kitendawili kwenye baadhi ya maeneo ya Nchi yetu. Serikali kupitia wizara ya mawasiliana na utamaduni iliwahi kukiri kutokuwepo Kwa mtandao hata wa kupiga simu kwenye vijiji zaidi ya mia nne. Na katika hivyo vijiji Kuna shule za sekondari na msingi nyingi sana.

Athari zake.
(A) Kwa wafanyakazi wa serikali. Wafanyakazi wengi hasa wa serikali wamekuwa wahanga wa tatizo hili. Nawekea mfano mdogo Kwa mwalimu ambae anatakiwa kila siku kupandisha(upload) kazi anazozifanya kila siku kwenye mfumo wa PEPMIS. Mwalimu analazimika kusafiri zaidi ya kilomita kumi (10) kwenda kutafuta mtandao ili walau aweze kupakia kazi za siku. Mda Anapenda kupakia(kuapload) hizo kazi vipindi vinakuwa havifundishwi Hali itakayopelekea kushukankwa ufaulu. Pia serikali imetangaza kupandisha madaraja Kwa walimu lakini kigezo namba Moja (a) ni mwalimu awe amepandisha angalau asilimia 60 ya kazi za mwaka. Je,serikali haioni kama inamwonea mfanyakazi huyu? Kutokupandisha sio kupenda Kwa mfanyakazi ila ni tatizo la mtandao kwenye maeneo mengi ya Nchi yatu.

Suuluhisho la tatizo
Serikali ifunge kwanza mtandao Nchi nzima Ili kumruhisu huyu mfanyakazi kufanya kazi katika mazingira wenzeshi. Pia serikali iangalie uwezekano wa kumpandisha mwalimu daraja sio tu Kwa kigezo Cha kufikia asilimia 60 ya PEPMIS Kwani itakuwa inamwonea mwalimu na wafanyakazi wengine.

Maoni yangu.
Serikali itafute wawekezaji Ili kuongeza upatikanaji wa network Nchi nzima. Isiwe inakimbilia kuvaa suti wakati nepi haijavaa!!! Maana yangu ni kwamba kabla ya kumlazimisha wafanyakazi wa serikali kujaza PEPMIS ilitakiwa iweke network Nchi nzima kwanza.
Ahsante.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom