kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kihistoria nchini Korea Mei 31 hadi Juni 6 mwaka huu kwa mwaliko wa Mheshimiwa Rais wa Korea, Yoon Suk Yeol, ziara ambayo ni hatua muhimu katika kuendelea kudumisha, kuimarisha na kuongeza ushirikiano wa moja kwa moja kati ya nchi hizi, ikiwemo kufungua milango kwa sekta binafsi ya Korea na Tanzania.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Rais anatarajia kufanya mambo makuu mawili ambapo Juni 2 atakutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea, na Juni 4 na 5 atashiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kati ya Korea na chi za Afrika; mkutano unaofanyika kwa mara ya kwanza kwa ngazi ya wakuu wa nchi na serikali, ambapo awali mikutano ilikuwa katika ngazi ya mawaziri na wataalamu.
Ziara hiyo inatarajiwa kuwa chachu na kutoa msukumo kwa wawekezaji kutoka Korea kuja kuwekeza nchini. Aidha, ushiriki wa Tanzania katika mkutano tajwa unatarajiwa kukuza uhusiano wa kimkakati; kupanua wigo wa biashara na uwekezaji; kutafuta namna chanya ya kukabiliana na changamoto za kimataifa; kutengeneza minyororo ya kimataifa ya usambazaji wa madini na nishati muhimu; na kujenga urafiki wa kudumu.
Wakati wa ziara, Tanzania na Korea zitasaini hati saba za makubaliano zitakazogusa sekta mbalimbali, kufungua soko la ajira kwa Watanzania nchini Korea, kuvutia wawekezaji wa Korea ili wawekeze katika soko la sanaa la Tanzania, kuanzisha ushirikiano na Kituo cha Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo wa Chuo Kikuu cha Korea Aerospace University (KAU) utakaosaidia kuboresha sekta ya anga nchini.
Tanzania na Korea zina uhusiano wa miaka 32 ambapo Korea ni nchi ya 12 kwa uchumi mkubwa duniani ambapo Tanzania ni kati ya nchi saba za Afrika za kipaumbele kwa Korea. Pia, kwa sasa Tanzania ni nchi ya kwanza kupokea kwa wingi misaada (ODA) inayotolewa na Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA) na ya pili kupokea kiwango kikubwa cha mikopo ya masharti nafuu (Concessional Loans), fedha ambazo zimekuwa na matokeo chanya kwenye ustawi wa kijamii na kiuchumi.
Aidha, Chuo Kikuu cha Anga cha Korea (Korea Aerospace University (KAU)) kitamtunuku Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honorary Degree) katika Usimamizi wa Sekta ya Anga kwa kutambua mchango wake katika mageuzi ya sekta ya anga ikiwemo kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege, kuwajengea uwezo watumishi na uongezaji wa ndege za abiria na mizigo.
Pia soma Ziara ya Rais Samia Korea Kusini itasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51