Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 270
- 362
Chini ya Rais Samia Suluhu, mipango hivi sasa inasukwa kati ya TANOIL, kampuni tanzu chini ya TPDC na Oman OQ ya Oman kufanya kazi kwa pamoja kwenye sekta ya kufanya bidhaa za Petroli.
Mpango huu umewekwa kazi wakati wa kikao kati ya Waziri wa Nishati, Mh January Makamba na Balozi wa Oman Tanzania Saud Hilal Al Shidhani. Mipango mingine pia ni kufanya kazi kwa pamoja kati ya Oman OQ na TPDC katika ujenzi wa mitambo ya gesi asilia.
Haya yote yanajiri hivi sasa baada ya safari ya Rais Samia Suluhu Oman Juni 2022 ambapo mikataba ya awali ilisainiwa huko Oman kati ya Tanzania na Oman. Ambapo mikataba hiyo si katika nishati tu, bali hata utalii, elimu na uwekezaji.
Hivyo ambayo Rais wetu Samia Suluhu anafungua nchi yetu, analeta fursa za uwekezaji ambazo ni kichocheo kikubwa cha ajira, kukuza pato la taifa na kuongeza biashara ambayo inaingiza fedha nyingi za kigeni ambazo ni muhimu sana katika kuimarisha uchumi wetu.