MAGEUZI KWELI
JF-Expert Member
- Jul 16, 2011
- 1,947
- 253
TANZANIA NA RASIMU YA KATIBA MPYA 2013
Si mbaya kwa watanzania kuwa na maamuzi makubwa ndani ya katiba wanayotaka iitawale nchi kwa sasa.
Ni jambo jema na wengi tumeona Rasimu na kwa mtizamo mkubwa sasa tunaingia katika mfumo wa serikali tatu.
Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunaona mfumo mpya unalisogelea Taifa maskini kabisa Duniani ambalo ni tajiri kwa Rasilimali ambazo zimeshindikana kuneemesha walio wengi na kuishia pasipogusika kwa namna moja au nyingine.
Kilio hiki kitadumu miongoni kwa wengi wasioiona faida ya rasilimali za Taifa.
SWALI LA KUJIULIZA KWA SASA:
Kwa umaskini huu ambao bado unalisumbua taifa maskini namna hii, kama Huduma za Afya Duni, Elimu isiyo na kiwango kabisa, Shule hazina madawati, Gharama za maisha ni kubwa sana, Shillingi kusidi kuporomoka thamani dhidi ya Dolla, Mishahara midogo, Vifo vya kuepukika, Mafisadi kulindana, Ajira za kujuana na wengi kuhangaika na elimu zao mitaani bila ya ajira NK..
Je ! > Tunaweza kuwekeza tena katika kuwa na serikali Tatu ambazo zitazidi kulikamua taifa hili kwa sababu ambazo bado hatujazitafakari faida zake na Hasara Zake?
Ø Kwa Tanzania hii hii na Zanzibar, Serikali Tatu msingi wake mkubwa ni kulisaidia nini taifa bila kuangalia uhusiano wa kihistoria ulioasisiwa na Waasisi wa Taifa?
Ø Uchumi uliopo sasa unaneemesha asilimia ngapi ya wananchi na baada ya mfumo wa serikali kupanguka wataneemeka kwa kiasi gani ili japo faida ya mabadiliko ionekane?
Ø Je Marais na Serikali zao wataligharimu taifa kiasi gani na ni vyanzo vipi vya mapato vinavyoweza lisaidia taifa hili ambalo bado linatia aibu kwa kukwapuliwa kwa Rasilimali zake bila ya woga wowote?
Ø NINI HASARA KWA SASA IWAPO SERIKALI ZITAAMUA KUACHANA NA MFUMO WA MUUNGANO NA KUJITEGEMEA KWA KUACHA MFUMO WA UJIRANI MWEMA KUSIMAMA KAMA TULIVYO NCHI ZA AFRIKA YA MASHARIKI AMBAZO MPAKA SASA TUNAJUANA NA KILA MMOJA ANAENDESHA MAMBO YAKE?
Ø Kwa mfumo huu hasara zake ni nini na faida zake kwa ujumla?
Ninalililia taifa langu maskini kutaka kuridhia Katiba (Muhimu sana)itakayoleta mtazamo mpya wa utawala kwa taifa maskini na kuanzishwa kkwa serikali zenye Gharama sana kuliko kinachohitajika kwa wananchi sasa.
SI MBAYA NIKIWA TOFAUTI SANA MTAZAMO WA WENGI, PESA NYINGI SANA ZITATUMIKA KULIENDESHA TAIFA NA SPEED YA MAENDELEO SIJUI ITAKUWA YA KASI GANI?
MUNGU IBARIKI NCHI YANGU TANZANIA KWA SASA BAADAE SIJUI ITAITWAJE MUNGU AJUA