Tanzania na Somalia zasaini mikataba ushirikiano wa ulinzi na usalama na kubadilishana wafungwa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Shirikisho la Somalia zimesaini Mikataba miwili ya makubaliano ya kushirikiana na katika masuala ya Ulinzi ma Usalama na kubadilishana Wafungwa.

Mikataba hiyo imesainiwa leo Januari 29, 2025, Jijini Dar es Salaam, upande wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa pamoja na Somalia, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Ahmed Moalim Fiqi.

IMG-20250129-WA1243.jpg
Akizungumza baada ya kusaini Mikataba hiyo, Bashungwa amesema Mkataba wa kubadilishana Wafungwa utaziwezesha nchi hizo mbili kuruhusu ubadilishanaji wa wafungwa ili waweze kutumikia adhabu katika nchi zao na kusaidia kupunguza gharama za kifedha za kuwahudumia wafungwa.

Soma Pia: Tanzania - Somalia zasaini hati nne za makubaliano ya ushirikiano

“Inapotokea kuna Watanzania wenzetu wameingia katika hali ya kuwa Wafungwa wakiwa kule Somalia, kupitia mkataba tuliosaini utatuwezesha kuwachukuwa Watanzania kuwaleta kwenye Magereza yetu, vile vile kwa Wafungwa wa Somalia watarudishwa kuendelea na vifungo vyao nchini kwao” ameeleza Bashungwa.

IMG-20250129-WA1241.jpg
Aidha, Bashungwa amesema Mkataba wa Ushirikiano kuhusu Ulinzi na Usalama, unalenga kuimarisha uwezo Vyombo vya Usalama kwa Kutoa mafunzo kwa Askari wa pande zote mbili, Kutekeleza Operesheni za pamoja, Kubadilishana utaalam katika masuala ya usalama na ulinzi pamoja na Kubadilishana taarifa za kiintelijensia.

IMG-20250129-WA1239.jpg
Kwa Upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa amesema utiaji saini wa mikataba hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muunga wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho ya Somali, Mhe. Hassan Sheikh Mohamud ili kuendelea kuimarisha ushirikiano.

IMG-20250129-WA1245.jpg
IMG-20250129-WA1247.jpg

IMG-20250129-WA1249.jpg
 
Hii itainufaisha zaidi TZ kwakuwa kuna wafungwa wengi wa kisomali wanaokamatwa kwa kuingia Nchini kinyume na sheria na kuishia kufungwa huku
 
TANZANIA NA SOMALIA ZASAINI MIKATABA USHIRIKIANO WA ULINZI NA USALAMA NA KUBADILISHANA WAFUNGWA.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Shirikisho la Somalia zimesaini Mikataba miwili ya makubaliano ya kushirikiana na katika masuala ya Ulinzi ma Usalama na kubadilishana Wafungwa.

Mikataba hiyo imesainiwa leo Januari 29, 2025, Jijini Dar es Salaam, upande wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa pamoja na Somalia, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Ahmed Moalim Fiqi.

Akizungumza baada ya kusaini Mikataba hiyo, Bashungwa amesema Mkataba wa kubadilishana Wafungwa utaziwezesha nchi hizo mbili kuruhusu ubadilishanaji wa wafungwa ili waweze kutumikia adhabu katika nchi zao na kusaidia kupunguza gharama za kifedha za kuwahudumia wafungwa.

“Inapotokea kuna Watanzania wenzetu wameingia katika hali ya kuwa Wafungwa wakiwa kule Somalia, kupitia mkataba tuliosaini utatuwezesha kuwachukuwa Watanzania kuwaleta kwenye Magereza yetu, vile vile kwa Wafungwa wa Somalia watarudishwa kuendelea na vifungo vyao nchini kwao” ameeleza Bashungwa

Aidha, Bashungwa amesema Mkataba wa Ushirikiano kuhusu Ulinzi na Usalama, unalenga kuimarisha uwezo Vyombo vya Usalama kwa Kutoa mafunzo kwa Askari wa pande zote mbili, Kutekeleza Operesheni za pamoja, Kubadilishana utaalam katika masuala ya usalama na ulinzi pamoja na Kubadilishana taarifa za kiintelijensia.

Kwa Upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa amesema utiaji saini wa mikataba hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muunga wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho ya Somali, Mhe. Hassan Sheikh Mohamud ili kuendelea kuimarisha ushirikiano.
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2025-01-29 at 15.07.19.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-29 at 15.07.19.jpeg
    367.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2025-01-29 at 15.07.21.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-29 at 15.07.21.jpeg
    442.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2025-01-29 at 15.07.23.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-29 at 15.07.23.jpeg
    497 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2025-01-29 at 15.07.26.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-29 at 15.07.26.jpeg
    328.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2025-01-29 at 15.07.28.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-29 at 15.07.28.jpeg
    247.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2025-01-29 at 15.07.34.jpeg
    WhatsApp Image 2025-01-29 at 15.07.34.jpeg
    300.4 KB · Views: 3
Back
Top Bottom