GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Katika Bara la Afrika lenye nchi 54, ni nchi chache tu, takriban nchi 10, ndizo zizsizokubali uraia pacha. Nchi hizo ni pamoja na Tanzania, Ethiopia na Congo D.R.C. Hata nchi jirani ambako baadhi ya Watanzania wamekuwa wakijinasibu kutaka kuhamia, yaani, Burundi, wametupiku katika hilo.
Lakini kwa nini Tanzania imekuwa miongoni mwa hizo nchi chache Afrika?
Inawezekana Serikali ina sababu ya Msingi sana kuung'ang'ania msimamo wake wa tangu zamani wa kutokuukubali uraia pacha. Na kama ndivyo, ni vyema ingeuweka wazi ili wananchi wote wazijue hivyo kuwa tayari kuitetea Serikali yao pale wanapozodolewa na "majirani" zao.
Na kwa kuwa sababu za msingi hasa haziko wazi, inaweza ikawa ni mojawapo kati ya hizi.
1. Watunga sera na Viongozi kwa ujumla Wana akili sana kiasi kwamba wanayaona ambayo wenzao wa nchi zilizoukubali hawayaoni, au:
2. Watunga sera na Viongozi wana fikra finyu sana kiasi cha kutotambua kuwa uraia pacha ni hitaji la wakati, hivyo si sahihi kupingana nalo.
Ipi hasa sababu ya msingi?