Tanzania na Uganda zapigwa marufuku na Ulaya kuendeleza Miradi ya Mafuta na Gesi

Hivi ndani ya bunge letu la michongo ni mbunge gani anaweza kujenga hoja juu ya hilo? Pengine kukaa kwao kimya kumeepusha aibu kubwa zaidi maana kama wangeongea hatuna hakika wangeropoka nini
Mh Lissu ameeleza katiba inasema nini ili Raia awe mbunge. Kigezo ninlujua kutambua a e i o u. Hao ndo tunaowatarajia wachallenge wenzao wa E U na kututungia mikataba
 
Hivi ndani ya bunge letu la michongo ni mbunge gani anaweza kujenga hoja juu ya hilo? Pengine kukaa kwao kimya kumeepusha aibu kubwa zaidi maana kama wangeongea hatuna hakika wangeropoka nini
Mbali ya kuwa vilaza, inawezekana pia kuwa wanaogopa kuwa wakionekana kuwa kimbelembele wanaweza kuwekewa vikwazo, wao wenyewe na watoto wao, mithili ya 'oligarchy' wa Urusi, wasikanyage huko majuu. Hili linawaogopesha sana wengi wao; mbali ya kutokuwa na uwezo wa kujenga hoja zinazoeleweka juu ya jambo lenyewe.
 
Mwana FA au Babu Tale wataweza kuongea nini kwenye hili? Ila yule mwendazake alituweza kwakweli
 
Kwani wao viwanda vyao haviharibu mazingira?
 
Mibunge dhalimu ya CCM imekaa kimya tu inapigapiga meza badala ya kutoa tamko kali kupinga kauli hizo za kikoloni
 
Mwana FA au Babu Tale wataweza kuongea nini kwenye hili? Ila yule mwendazake alituweza kwakweli
Mwendazake katuachia msala, alitaka kujitengenezea bunge ambalo litakuwa likilamba viatu vyake 24/7 na kutawala maisha yake yote. Na kweli ametawala maisha yake yote hahaha... God is great
 
Ile sera yetu ya kutofungamana na upande wowote ni sera ya kijinga, na kivivu sana, inatufunga mpaka midomo na akili tushindwe hata kujitetea pale inapoonekana wazi maslahi yetu kiuchumi yanataka kuvurugwa na hawa wazungu.

Namkumbuka JPM wakati akianzisha mradi wa Nyerere Dam, zilipigwa kelele kama hizi, lakini aliziba masikio akaendelea na ujenzi wake licha ya kuonekana kichaa kwa baadhi ya watu, hawa wazungu wanatakiwa kuijua misimamo yetu ili wasiendelee kutuchezea.

Lakini kwa huu utawala wetu wa sasa, unaojipambanua "kufungua milango" na "kutafuta misaada ya masharti nafuu" siwaoni kama watakuwa na kiburi cha kulaani hilo tamko, wazungu wakati mwingine wanamhitaji kiongozi jasiri wa kuwaambia ukweli bila kuwaficha ndio hurudisha heshima.
 
Mshana Jr Soma Tena vibesen xxx mkwepu jr bagamoyo mjingamimi Mzee Wa Kazi Chafu
 
MRADI WA KUTOA MAJI ZIWA VICTORIA KUJA TABORA waliupinga kwamba utaua Mto Nile tukakomaaa Mradi Ukajengwa na leo Maji yanatumika Shinyanga na Tabora na huenda yatafika Dodoma Hongera sana kwa Mhe. EDWARD LOWASA Waziri wa Maji wakati huo alitoa Press ya Kibabe sana sana ambayo naaamini ilikuja kumbeba baadae kuwa PM.

MRADI WA BWAWA LA NYERERE ULIPINGWA SANA SANA MPAKA KUTISHIANA VIKWAZO nk HONGERA KWA JPM MWAMBAAAA alikomaaa na MRADI UTAKAMILIKA INGAWA VIBARAKA WALIOBAKI WANAUHUJUMU MRADI UONEKANE WHITE ELEPHANT.

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA ndicho kipimo sasa cha WALAMBA ASALI WA MAKUNDUCHI ndio tutajua wanatufaaa 2025 au Ndio tiketi yao ya kushindwa. Ila angekuwepo Mwamba wa Chato najua leo leo angetoa tamko la Kibabe mpaka maombolezo ya Buckigham yaonekane machungu
 
Halafu mtamuuzia nani hiyo crude oil ?
 

Hapa ndo naona umuhimu wa Magu
 
"Kula uliwe" - Kikwete.

Dunia ya leo wewe kinyangarakata ukijifanya mroho na kutaka kula peke yako, shibe itakutokea puani. Tusisahau yaliowakuta GHddafi na Saddam Hussein. Kosa lao lilikwa ni kukata mirija tu.


Tanzania inatakiwa tusikurupuke, diplomasia ya hali ya juu itembee, na naamini tuna wana diplomasia waliobobea ndani ya Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…