Tanzania na Urusi kushirikiana katika kueneza lugha ya Kiswahili

Tanzania na Urusi kushirikiana katika kueneza lugha ya Kiswahili

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan ambapo wamejadili namna bora ya Tanzania na Urusi kushirikiana katika sekta ya Utamaduni na Sanaa kwa manufaa wa wananchi wa pande hizo mbili.

Akiongea wakati wa kikao hicho kilichofanyika Juni 21, 2023, Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema Tanzania na Urusi wataendelea kushirikiana katika eneo la Utamaduni na Sanaa kwa kuzingatia uhusiano wa muda mrefu ulipo baina nchi hizo mbili katika masuala mbalimbali ikiwemo lugha ya Kiswahili.

“Tunatambua juhudi zinazofanywa nan chi ya Urusi kwa kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili, sisi tupo tayari kupitia BAKITA kutoa vitabu vya kujifunzia Kiswahili, tutatoa vitabu kwa walimu wa Kiswahili kutoka Urusi ambao watakuja hapa nchini wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani Julai 7 mwaka huu ili vitabu hivyo viwe nyenzo nzuri ya kufundishia lugha ya Kiswahili Urusi” amesema Bw. Yakubu.

Kwa upande wake Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan amesema nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ambapo wataendelea kutoa nafasi kwa Watanzania kusoma nchini humo ambapo watajifunza pia lugha ya Kirusi ili kuendeleza mahusiano ya kibiashara na uchumi hatua inayoongeza nafasi kwa Watanzania kufanya kazi Urusi na Warusi kufanya kazi Tanzania.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bi. Consolata Mushi amesema watashirikiana na Ubalozi wa Urusi nchini ambapo wafundisha maafisa wa Ubalozi huo lugha ya Kiswahili kwa wageni na watashirikiana nao kufundisha wataalam wa tafsiri na ukalimani hatua itakayosaidia kueneza lugha ya Kiswahili duniani.

IMG-20230621-WA0270.jpg
IMG-20230621-WA0268.jpg
IMG-20230621-WA0269.jpg
IMG-20230621-WA0271.jpg
IMG-20230621-WA0272.jpg
 
Mambo ya kijinga
Baada ya kuendeleza technology na biashara eti mnaendeleza kiswahili
 
Mambo ya kijinga
Baada ya kuendeleza technology na biashara eti mnaendeleza kiswahili
Biashara ya utumwa ikirudi naamini utakuwa wa kwanza kuuzwa maana huthamini hata kilicho chako.

Kiswahili ni chako na Cha kujivunia Popote na yote hayo unayosema yatakuwa bora zaidi kama tukihimiza matumizi ya Kiswahili.
 
Back
Top Bottom