Nasema walau Raisi Mkapa alikuwa anatoa data za kumwezesha mtu kuchambua mambo. Hapa kwa masaa zaidi ya 3 porojo tuu!!! mtu utachambua lipi? maana hata aliyosema mwanzo mtu umeshasahau. Hii inasikitisha sana. Watanzania kazi tunayo, tena kubwa sana.
Tunahitaji mwelekeo mpya kabisa, ambao katika hii hotuba sijauona hata kidogo. Ndio Tunajua tumetoka wapi, Tulipo tunapajua (kwani machungu yake ni makubwa), sasa tuonyeshe wapi tunaelekea, hakuna kitu.
Jamani nasema huyu dereva wetu sio kwamba tu hajui njia ipi yakupita (ambalo ni tatizo dogo tu, akikubali kupokea ramani) bali hajui wapi tunapokwenda. Hivyo tatizo kwake sio njia bali ni wapi atupeleke. Huu ni muda muafaka wa kumwambia akae pembeni maana akifitufikisha pabaya hata ukimwondoa na gari tunaweza tusiwe nalo tena.
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake, waone ya kwamba dereva hafai ni wakubadilisha