Tanzania National Identities (Vitambulisho vya Taifa)

Hivi hazina kuna Account? Maana nimesikia kwenye hotuba ya Raisi kwamba hizo fedha ziko kwenye account hazina, wakati ninavyo elewa fedha za serekali zinatakiwa kuwa Bank. Iwe Bank kuu kama government Bank na central Bank au hizo bank Zingine NBC/NMB/CRDB/ etc
 
Jamani EPA hizi ni outstanding LC! ambao hamjaelewa semeni tufungue darasa.

Zinaposemwa kuwa ni fedha za wananchi/serikali ni kuwa ule wizi na kugushi kote kulikotokea, kama wadai wangekuja kudai siku moja kudai malipo yao ni wazi kuwa serikali ndio ingewajibika kulipa kutoka kwenye hela za walipa kodi kwa sababu ndio ilikuwa na dhamana ya kuzitunza.
 
Siku hizi sina mda wa kupoteza kusoma rai. Halina tofauti sana na Uhuru au Mzalendo. Halina umaarufu tena na ndo maana waandishi makini wameliacha. Ni la fisadi mkuu Rostam.
 
Nilifurahishwa na maneno yake kuwa Mafisadi wa EPA wamefilisiwa na mali zao kushikiliwa, na wakati huo huo anasema kuwa amewapa muda wa kulipa fedha hadi October 31, sasa swali hapa ni kuwa hawa jamaa watatoa wapi fedha za kulipa kama hata mali zao zimeshikiliwa?

Wataweza kupata mkopo kwa kuweka dhamana gani?

Kweli JK ni kiboko.
 
Huu ni mwaka wa shetani kwa Mafisadi watajitahidi sana kumsafisha mzee ili asikamate mali zao kama kweli ana nia hiyo ,ila nguvu ya umma itatamalaki daima.

Mtachapa sana matoleo mengi ila kama mafisadi wa EPA hawajafikishwa mbele ya sheria hataweza kutakata daima, hata kama mtamuweke kwenye povu la geisha.......
 
Ama kweli mswahili ame-frustrate kila mtu.



.

Duuu..hii kitu imeniletea mfadhaiko wa akili bila kutarajia.

Nilipoteza muda mwingi kumsikiliza, as a result tangu pale nilishindwa kabisa kuendelea na kazi.
Unfortunately mpaka sasa sija-recover bado nina msongo wa mawazo.
 
Ni kupoteza muda bure kuwalaumu RAI kwa hili, wako pale kwa ajili ya mambo kama hayo. Kama kuna mtu anategemea RAI watailaumu serikali ya JK, basi huyo mtu ni very naive.

Ni sawa na kutegemea gazeti la uhuru limshambulie JK au Makamba.

Ni sawa na kutegemea Tanzania Daima limshambulie Mbowe.

Kwanini kupoteza muda kufuatilia magazeti ya propaganda? Mimi hayo magazeti hata nipewe bure, bado siyataki.
 


Hii nayo VIPI katika THISDAY?

http://www.thisday.co.tz/News/4444.html

 

Mimi nadhani, Uhuru/Mzalendo na Tanzania Daima ni afadhali sana tena mara milioni, lakini magazeti ya Rai na Mtanzania, haswa Rai yamepoteza mwelekeo na hayana sababu ya kufanya hivyo zaidi ya kujipendekeza.

Hii ni hatari sana kwa USALAMA WA TAIFA letu... tuendako ni kubaya sana. Mungu atatunusuru
 

Rostam ni Mwandishi? acheni upuuzi wenu... kuwadanya waTanzania... acheni wachambue wenyewe.
 
Rostam ni Mwandishi? acheni upuuzi wenu... kuwadanya waTanzania... acheni wachambue wenyewe.

Kashehe umepatia, tena kwa ushahidi ni kwamba Gazeti la Mtanzania Jumapili Agosti 24 (leo), limetoka na kichwa cha habari "Dk. Slaa amvaa Kikwete, asema hakustahili kugawa fedha, ahofia mdudu wa kiinimacho, sasa zasubiriwa siku 68 za fainali, ama zitamshusha ama kumpaisha" wakati huo gazeti la chama la Mzalendo la Jumapili Agosti 24 (leo) nalo lina habari kubwa isemayo, "Hofu ya mafisadi EPA kutoroka yatanda" ni kutokana na muda mrefu aliotoa JK kurejesha.

Kwa maoni yangu ni kwamba, pamoja na matatizo ya wamiliki wa magazeti akiwamo RA, waandishi wetu ndio wa kulaumiwa ama kupongezwa kwa ujinga/ujanja wao na mfano ni magazeti hayo ya leo likiwamo la Chama (CCM).
 
Tutakuwa pamoja!!! Ningekuwa mimi mmiliki wa Radio za Tanzania, ningeibia matangazo na kuyarusha, lakini mhnnnn, tumelala siku zote
 
Watanzania Wenzangu,

Baada ya Muungwana kumaliza kusoma Bajeti yake,Mzee Mwanakijiji alitoa rai ya kusita kuandika tena hapa JF mpaka hapo mtu mwingine atakapofikisha post 11,000.Ila baadaye Mzee Mwengangu alirudi na kuendelea kuandika sababu ya uchungu aliokuwa nao kwa ajili ya watanzania wote.Nampongeza kwa hilo!

Toka Muungwana amalize Hotuba ile nimekuwa nikipitia kila kipengele cha hotuba ya masaa manee aliyoyasoma Muungwana,wakati huo huo nikilinganisha na hotuba mbali mbali za wizara za serikali.Alichokizungumza kuhsu kilimo,Madini,maji,mazingira na khali ya uchumi wa nchi hakuna tofauti na kile walichozungumza Mawaziri.

Ukiangalia kwa undani zaidi,watu hawkutegemea hotuba ya namna hii,hata mimi mwnaa CCM nilichukizwa nayo,siyo tu kwasababu ya urefu wa hotuba ile bali mambo yaliyozungumziwa mle ndani.mkulu alishindwa kutupa maji ili kupoza kiu tulichonacho.Hii inasikitisha sana na hasa maneno kama haya kuwa yeye ni Tumaini lilolerejea.

Nimefikira sana,inaonesha Mkuu hana uwezo wa kutatua mambo magumu,ameshindwa kutuambia ni lini bei ya mafuta itashuka ili tuweze kuwa kama nchi jirani za kenya na rwanda.AMeshindwa kusemea kusitishwa kununuliwa kwa magari ya kifahari ili khali walimu wakishindwa kulipwa mishahara yao.

Watanzania wenzangu,kipindi flani niliwahi kuhisi na kukubali kiaina kuwa yawezekana Muungwana anadanganywa na wasaidizi wake ila ana dhamira nzuri kwa watanzania ,na hii niliijenga baada ya yeye kuzoea kutuzuga na maneno haya "Tanzania yenye neema inawezekana".Toka Suala la RDC Niliweza kugunduayeye ndiye anatudanganya sisi na wala siyo wasaidizi wake.Mkulu amsehindwa kutupa majibu ya maswali rahisi sana,

1.Je nini kitafuata baada ya mkataba wa DOWANS kuvunjwa?
2.Je baada ya kamati ya madini kuamliza kazi yake,ni lini mikataba hii itafanyiwa kazi na kunufaisha watanzania?
3.Waliohusika na RDC watachukuliwa hatua zipi za kisheria,Hasa Nationa Negotiation team?(Mawazo ya kina Mwakyembe yametupwa??)


Tumekuwa watu wa kuzugwa kwa kutumia kamati ambazo kila siku zinaendelea kutafuna pesa yetu na ripoti hazifanyiwi kazi.Kamati hivi zinatumia pesa nyingi sana na watu huwa wanalipwa kwa siku wastani wa sh. 400,000 hadi 500,000 kwa ajili ya vikao vya kamati huku wakikaa katika hoteli za kifahali maneno ya bagamoyo.Kamati zinafanya kazi ila HATUA hazichukuliwi.Tuliona tume ndogo tu ya miezi mitatu ya kesi ya kina malima na Mengi ilitumia zaidi ya milioni 100.Je kamati za miezi sita hutumia kiasi gani?

Mwaka Jana nilipokuwa Bungeni,niliwahi kumuuliza kiongozi mmoja wa wizara moja ya serikali,Je ni kiasi gani huwa kinatumika kwa jili ya wizara kuja kuwasilisha bajeti.Yaani kuanzia maandalizi hadi sherehe ya mwisho bajeti imepitishwa.Aliniambia ni zaidi ya milion 600.Je kuna wizara ngapi?hizo ni takribani ya bilioni 30 ukijumlisha na posho za wabgune hutumika kwa akili ya kikao kimoja tu cha bajeti.unadhani kiasi gani cha pesa kinapotea?Ndiyo kuna umuhimu,ila kuna haja gani ya kutumia pesa zote hizi..basi tuwe na kikao kimoja cha bajeti kila bada ya miaka 3!

Tumekuwa waoga sana,tumekuwa wavumilivu wajinga tusitaka kuchukua hatua za kufanya,saa ya ukombozi ni sasa na ingekuwa vyema tukaandamana na kumuunga mkono spika ya kuwa wahujumu uchumi hawatakiwi kuonewa Huruma hata kama ni rafiki zake na Mkulu.Tayari Mkulu ameoneshwa kuchukizwa kwake na spika kufanya majumuisho ya hotuba yake kwa muda wa dakika kumi.Wachunguzi wa mabo wanaelezea pia hata kauli ya spika kutoa mwanya kwa wabunge kuijadili hotuba hiyo kumezua mgongano mkubwa katia ya spika na serikali.Serikali inahoji kwanini wabunge WAJADILI mambo yaliyosemwa na Mkuu wa nchi?

Tumeshakata tamaa vya kutosha,na sasa ni wakati wa kuchukua HATUA ili kuikomboa nchi yetu,tutumie sanduku la kura kuweka viongozi makini na walio na uchungu na nchi yetu.Hii changamoto ianzie katika vyama vyetu kwa kuwakata wale wote wasiyo na machungu na nchi yetu na tuwape wale wanaotaka kufanya yale tuyatakayo.Tutoke kuzimu na tuache kuwa mazezeta hata kama wanatuona mandondocha.

Yes I have said,ni bora kuishi bila yeye ,sababu ameshindwa kutupa yale tuyatakayo.chukua HATUA kwa kuanza kujipanga mapeama sasa ili tumpate yule tumtakaye.tutumie njia iliyo sahihi na ambayo ni haki yetu.WE SHOULD STOP TO MONITOR OUR GOVERNEMENT AND START PARTICIPATING IN CHANGING OUR COUNTRY.

Nasita kuandika mpaka pale uchaguzi wa TARIME utakapoaanza,ki -ukweli Jk ameniangusha sana kwa kushindwa kuchukua HATUA kwa watu wa EPA.Nitaendelea kuwa msomaji tu huku nikitafakari 2010.
 

JK alidhani anahutubia genge la vilaza wenzake wa CCM , kumbe kulikuwa ni mchanganyiko wa wajanja na vilaza wengi wa CCM Bungeni ambao makofi walikuwa wanaya mwaga tuuuuuuuuuuuuuu
 
Nadhani miezi miwili waliyopewa mafisadi wa EPA si mingi, na wasiwasi kama kweli JK ataishia kurudisha pesa huku akijua macho ya watanzania (plus wafadhiri)wengi yapo huko, unless kwenye mbinu za medani jeshini awe alipata negative.

JK (inawezekana) anajua kuwa kukimbilia mahakamani kutachukua miezi kama siyo miaka kadhaa hadi hukumu itolewe, nakuipata hiyo hela pia kutategemea mshitakiwa kushindwa kesi. Je hakimu akisema mharifu alipe baada ya kutumikia kifungo cha miaka 15 jela? Asubiri mpaka 2025 kuipata? ndio hao akina kiula walipelekwa mahakamani na wakachomoka!

Hao waliotajwa kuwa wamegushi, si ajabu nusu wakachomoka (kushinda kesi) pia, ukiwa na vijisenti unatafuta wakili wa nguvu na ukikuta mwendesha mashita mchovu unamlainisha kirahisi tu. So kama hesabu zake ni kuvuta kwanza huo mshiko, then ndio awaburuze mahakamani...atakuwa kapiga bao la kisigino.

Kama shida yake ilikuwa kukusanya tu hivyo vijisenti basi hakukuwa na sababu ya kuwatuma Mwema, Hosea na Mwanyika kufanya kazi hiyo..... Kuikomalia serikali ili ipambane na mafisadi ni muhimu lakini mbinu na maarifa zinatakiwa....TZ ina matatizo mwengi, kama dila tulishapoteza toka zamani jamani, tusingekuwa watatu toka mwisho kiuchumi pamoja na resource zote hizi.....tuangalie tatizo kwenye historia nzima ya TZ kama kweli tunataka kufanikiwa, hata hivyo huu ni mwanzo mzuri....
 
rostam usijali wewe ni muwekezaji mzalendo hupeleki mali nje kama chenge tutakuunga mkono mpaka anguko lako na mwishi
.Ninadhani hao wengi walikusema ni walewale.Madikteta ambao wako ngambo ya pili wa jamhuri ya muungano.

Kwani hawa jamaa kila wanaloliona/kutaka wao wanadhani ni sahihi uchukie kama wanavyochukia wao.Naamini hawa watu wakiwa watawala hawatakuwa tofauti na De Klerk au mugabe. Wana JF lazima tukubali mawazo tofauti.

Rostam anabambikwa kwa ufisadi lakini Hakuna aliyethibitisha kimazingira au ushahidi bayana. Hivi rai kusifia hotuba ya JK kwa mtazamo wao kuna kosa gani.wawache wasome wale wanaolingana nao. mimi nimekwisha lisahau katika kumbukumbu zangu.
 
Kama mipango itakuwa mizuri matangazo hayo pia yatarushwa na Bongo Radio. Stay tuned.
Wote mnakaribishwa.
Mkuu jaribu kuungana na Bongo radio naona site yako ina pop up nyingi kwa wanaotumia exproler inakuwa kero.......tunamsubiri SS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…