Mpango huu tumeuzungumzia sana hapa kijiweni na hakika inaonyesha wazi wengi wetu wanachopinga sii kuwepo kwa vitambulisho isipokuwa gharama ya Vitambulisho hivyo. Binafsi baada ya kuuona mfumo mzima wa Kiutawala hapa Tanzania nadhani swala hili linahitaji kutazamwa upya kwa sababu zipo njia rahisi na muhimu kupata faida zote za Vitambulisho.
Kwa mfano hadi sasa hivi swala la wananchi kuwa na Social Security ambayo naweza kuifananisha kwa ukaribu (Tanzania) na Tin number - HALIPO. Sababu sielewi kabisa ikiwa kweli serikali yetu inataka kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Binafsi naamini kabisa kabla serikali yetu haijafikiria kutoa vitambulisho ni muhimu kwanza ihakikishe kila mwananchi apatiwe tin number iwe wewe raia ama sii raia wa nchi hii ili kuhakikisha Ukusanyaji kodi na mafao mengine ya kitaifa yanapitia namba ya kodi ya kila mtu.
Ni maajabu ya Mussa kuona kwamba Mtanzania mwenye tin namba ni yule tu anayejihusisha na biashara ama malipo fulani ya kodi za serikali, laa kama huna uagizaji wa mali basi wewe huna ulazima wa kuwa na tin namba. Hii hakika hainingii akilini kabisa kwani umuhimu wa wananchi kupewa tin namba ni mkubwa zaidi ya hivyo vitambulisho na pengine kuna wananchi wengi wasiookuwa na tin namba kuliko waliokuwa nazo! kisha tunajisifia kwa mfumo wetu wa ukusanyaji kodi...Halooo!.
Watu hukatwa ama kupokea kodi na malipo mengnineyo kwa kutumia tin namba zao..hii ndio nguzo mojawapo kubwa ya ujenzi wa maendeleo ya nchi yeyote iweje kwetu kiwe ni kitu kisichokuwa lazima?Tin namba itarahisisha sana ukusanyaji wa kodi na kufahamu nani hajalipa au kuwakilisha claim ya kodi ya mwaka na pia mwaka gani, iwe hata watu wawili au mia wanafanana kwa majina...
Leo hii wapangishaji majumba hawalipi kodi lakini kama Tin namba itatumika kulipia pango kwa kila mpangaji sijui hao wenye kupangisha wataepa vipi kodi. Muhimu pasiwepo na urasimu maanake Bongo hakika imefika ktk hatua nyingine ya Ufisadi - Urasimu...hili ni gonjwa jipya kuliko ukimwi lisiloweza kupata tiba bila kumpata mtawala Dikteta...Wakuu zangu na wa Waheshimiwa tuwe na imani na nchi yetu, tuwe wakweli na wenye uzalendo kuweza kufuata taratibu za usajili wa wananchi ambao unaweza kufanya kazi kwa malengo bora zaidi..
Siku zote ngoma huanzia hapa kwenye vitambulisho vya kodi. Hata wale waliokwenda Ulaya watakubali na maneno yangu kwani wao pia hulazimika kwanza kupata namba ya kulipia kodi hata kama hawana vitambulisho vya kuishi nchi hizo na ndio pekee vinavywawezesha kupata ama kufanya kazi nchi hizo, pasipo namba hizi huwezi kuajiriwa kabisaaa pamoja na kwamba unaweza kuwa na kitambulisho cha Utaifa. Hivi ni vitu viwili tofauti na tin namba kwa kila mwamamchi ndio hutangulia hivyo vitambulisho vya Uraia..
Hivyo naiomba serikali yetu bila kupoteza muda, fedha na kwa urahisi zaidi kuanzisha kampeni ya wananchi kujiandikisha kupewa namba za tina iwe hata mtoto mdogo na namba hivyo ndizo pekee zitakazo mwezesha mtu kupata kitambulisho cha Uraia pindi itakapo fikia wakati wake..
Huu ndio utaratibu unaoelewaweka na wenye kugharibu fedha ndogo sana. na tusiseme haiwezekani kwani kama mashirika ya simu yameweza kuwalazimisha watumiaji wote wa simu kujisajili sidhani kama itakuwa shida kubwa kwa serikali yetu kulazimisha wananchi wote kujisajili ili kupata tin namba kwa majina yao (personal) na biashara zao, kisha ndio mpango wa vitambulisho vya Uraia vitafuata.