Tanzania nchi ya maajabu: Mjue Mtanzania wa kwanza kucheza kombe la Dunia Urusi 2018

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,491

Anaitwa Yussuf Yurary Poulsen mwana wa ardhi ya Tanzania na Denmark, ambaye ni mcheza soka maarufu nchini Denmark, aliyetajwa kuongoza kikosi cha timu ya Taifa ya Denmark ambako ndiko alikozaliwa na kuishi.

Yusuph alizaliwa Juni 15, 1994 huko Copenhagen nchini Denmark, huku baba yake akiwa ni Mtanzania mwenyeji wa Mkoa wa Tanga, anayeitwa Shihe Yurary aliyekuwa akifanya kazi kwenye meli ya mizigo, ambayo ilikuwa ikifanya shughuli zake kati ya Afrika na Denmark, na mama yake anayejulikana kwa jina la Lene ni raia wa Denmark.

Kupitia kazi zake hizo, Shihe alikutana na Lene na kuanzisha uhusiano uliomleta duniani Yusuf, na akaamua kuhamishia makazi yake jijini Copenhagen, Denmark ni raia wa Denmark.

Yusuf alianza kucheza soka akiwa mdogo, na kujiwekea rekodi mbali mbali mpaka kusajiliwa na timu ya RB Leipzig ya nchini Ujermani, ambako bado yupo mpaka sasa.

Kwenye timu yake ya Taifa ya Denmark Yusuf anacheza nafasi ya mshambuliaji, ambayo ni maalum kwa kufunga magoli, na imetajwa kushiriki kombe la dunia mwaka 2018, ambaloi linatarajia kuanza siku si nyingi nchini Urusi.
 
Ni mtanzania au ana asili ya Tanzania!
 
Maajabu ya tanzania yako wapi hapo
 
Shida kubwa sis tulio nayo wenye vipaji tunawapiga sana mawe yani wewe ona hata huyu Rais wetu pamoja na kujitoa kwake kote they wish hata kesho afe sijuwi nani katuloga ila Mungu atatutetea.
 
kama huna akili ya utambuzi si rahisi kufahamu....
bora nibaki hivi kutokuona maajabu yoyote hapo ya tz.thiago alcantara baba ake ni mbrazil ila yupo hispania.
 
bora nibaki hivi kutokuona maajabu yoyote hapo ya tz.thiago alcantara baba ake ni mbrazil ila yupo hispania.
Hata Deco alihama nchi
 
Huyu sio mtanzania. Ni m-danish mwenye asili ya tanzania.

Watz kwa kutamba hatujambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…