philosophy
Senior Member
- Nov 11, 2012
- 104
- 42
Katika kipindi hiki; ni kipindi cha mpito kwa watanzania. Hii ni kwa kuwa watanzania wengi kwa uzalendo wao wamejikita katika kutafuta mustakabari wa taifa hili kwa tashwishi kwa kudhani kuwa ndilo sululisho la maisha ya watanzania na Tanzania waitakayo. Jambo ambalo mimi ninalishuku!
Kwa mujibu wa Kamusi ya Babyloan( ya kiingereza), inaeleza kuwa Demokrasia ni serikali inayoendeshwa na watu wa nchi; nchi yenye serikali ya namna hii; jamii yake au watu wake wanakuwa na haki sawa na upendeleo hasa uliokitwa kwa maamuzi ya wananchi/rai wenyewe. Dekorasia ni zaidi ya utawala wa kiserikali, ni hadi kwenye maamuzi ya walio wengi na mabao pasi na kujali ni wa aina gani almradi ni timamu; wasemalo na kuliamua ndilo linakuwa. Hivyo, nguvu ya maamuzi ipo mikononi mwa wengi. Wakati huo huo, Katiba ni sheria, utawala/mamlaka au muundo wa kanuni za utawala. Kwa mantiki hii, katiba ni sheria mama kama si baba ambazo zimehifadhiwa ama kwa maandishi au pasipo maandishi kama mwongozo wa utawala katika jamii fulani au nchi/taifa husika. Kutokana na katiba sheria nyingine ndogo ndogo za nchi zinaundwa na chombo chenye malaka hayo.
Katika rasimu hii ya katiba mpya, hasa rasimu ya pili, kumetokea masigano baina ya makundi mbalimbali, yakiwemo ya siasa, n.k. Katika jambo hili, imeonekana kuwepo na nyufa nyingi sana kwa mtazamo wa wanaodai katika mkondo huo; huku ikionekana katiba hii haikidhi au haikufuata matakwa ya wananchi. Ila jambo, kushangaza ni kuwa, rasimu hii haikukidhi matakwa ya watanzania walio wengi au haikukidhi matakwa ya watanzania walio wachache na wenye maslai yao binafsi juu nchi hii? Swali ambalo sijalipatia majigu sahihi hata kama yatapatikana ninasita kukiri kuwa yataniridhisha ni kuwa, inakuwaje tume ionekane haijafuta maoni ya watu kwa maana kuwa imejiwekea ya kwao huku, tume hii imekusanya maoni ya watanzania na kunakili kila maoni yaliyotolewa na kila mtu na mimi nikiwa ni mmoja wapo, wakati huo huo kamati hii ilikuwa ilikutana na rais na baadhi ya viongozi na taasisi mbalimbali na kuridhishwa na kazi yao? Lakini hapo hapo tume hii imetumia mfumo wa demokraia, ambao unawataka wachukue maoni ya msingi na muhimu ambayo yameonekana kuelezwa na watanzania wengi, dukuduku yangu ni kuwa inakuwaje baadhi ya maoni yasiwemo wahusiak walalamike? Pengine maoni yao hayakuwa na mashiko lakini bado wingi wa walioyatoa yawezekana kuwa ni kiduchu, na kwa misingi ya demokrasia na kwa kulijua hilo kwa nini wahusika walalamike? Basi kama ingelikuwa hivyo basi kila maoni yangeliandikwa na nina mashaka bado kama katiba hiyo ingelisheheni yote hayo na ingelikuwa ni katiba ya wapi hiyo kama si ya mbinguni!
Yamezuka maoni ya kwamba tume ya katiba haikuonesha mbinu za kisayansi ambazo imezitumia kupata hayo maoni, hasa kelele nyingi zikiwa ni serikali tatu. Je, tume hiyo imewekwa kwa mujibu wa sheria na shria hiyo ina kifungu kinachowataka waoneshe mbinu hasa za kisayansi walizotumia kupata hayo maoni? Kama ni hivyo na hawakufanya hivyo, tume imeenda kinyume, lakini kama hakuna sheria iliyowataka wafanya hivyo, nachelea kuhukumu uwezo wa kufikiri kwa wenye kudai hivyo, kama ni wa kiasi gani. Mbali zaidi ni suala la serikali tatu; iankuwaje suala hili lionekane kama lina mashiko kwa baadhi ya watu na lisiwe na mantiki kwa baadhi ya watu, wakati maoni hayo yalitolewa na watanzania walio wengi kwa mfumo wa demokrasia? Hoja hii inatoka wapi ya kwamba serikali tatu ni mbovu,serikali mbili ni muhimu wakati watanzania wao wenyewe waliopewa nafasi ya kutoa maoni wameichagua hoja ya serikali tatu? Ni kwa nini ionekane rasimu hii ina mapengo, na wenye kuyaona hayo mapengo walikuwa wapi kabla ya rasimu ya pili kutoka? Kuna haja gani ya baadhi watu fulani, kushawiahiwa hata kama kwa hoja kuhusi kipegele fulani wakati kipengele hicho kimependekezwa na watanzania walio wengi? Mwisho, ninashuku kama kweli katiba hii tunayoitaka kama kweli itakiwa na watanzania wote kama si baadhi ya watanzania: kwani; mimi, tofauti na taasisi za kisiasa na nyinginezo kuja na maoni ya katiba mpya, sikuwahi kusikia kuwa angalau mkoa fulani au mikoa fulani kwa mfano, wametaka kuwa na katiba mpya!
Ngoja niishie hapo kwa leo, ninayo mengi ..
HITIMISHO NITALITOA BAADAE