SoC04 Tanzania nchi yangu

SoC04 Tanzania nchi yangu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Abu atiqah

Member
Joined
May 24, 2024
Posts
17
Reaction score
8
Utangulizi:
Tanzania ni nchi ambayo imepewa zawadi ya kipekee na Mwenyezi Mungu katika bara la Afrika kwa kubarikiwa kuwa na sehemu nyingi zenye vivutio na rasilimali ambazo zikitumika vizuri zitaongeza Pato la Taifa. Nchi hii imekuwa maarufu duniani kutokana na Mlima mrefu barani Afrika, kisiwa na sehemu ya kuvutia Duniani zanzibar, madini ya Tanzanate na mbuga za wanyama zenye kuvutia zaidi duniani.

Sauti ya mabadiliko katika kipindi cha miaka 5 na kuendelea imepewa jina la Tanzania nchi yangu ambayo itaangazia mabadiliko ya kweli kwanzia kuwajenga wananchi wake kutumikia nchi yao kwa uadilifu na uwajibikaji wa kweli ili kukuza uchumi wa nchi ambao tunaitarajia ndani ya miaka 5 kwa kutumia tunu za rasilimali ambazo tumebarikiwa kwazo.

Mabadiliko haya yata angaza katika muundo wa shughuli za kiuchumi kwa kuboresha sekta kadhaa ndani ya serikali yatu ili kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa kama ambayo hivi sasa kumekuwepo na mfumuko wa bei dunia kwahiyo na Sisi kama nchi lazima tuwe na mipango madhubuti kudhibiti na kuendana na hali hii ili nchi yetu fedha zake zisishuke thamani na watu wake wasishindwe kumudu gharama za maisha.

Shabaha kuu
kutumia rasilimali tulizokuwa nazo kujitegemea na kujiimarisha kiuchumi

Shabaha ndogo
Kuimarisha sekta mbali mbali kila mwaka zichangie ongezeko Pato la taifa 1.5% hadi 2%.

Malengo ya mabadiliko
  1. kukua kiuchumi
  2. Kuondoa kero za ajira
  3. Kuimarisha Elimu na kuwajengea uwezo wahitimu
  4. Uzalendo na kujituma kwa watendaji
Maono
Ndani ya miaka 5 hadi 15 na kuendelea Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi ambazo zitakuwa zinatumia rasilimali zake 100% kwaajili ya makadilio ya bajeti ya nchi.

Muundo wa mabadiliko katika sekta za serikali.
imekuwa ni mazoe ya watendaji kutenda hovyo na wanasubilie mwisho wa mwezi wapate. Dhana ya uwajibika na uzalendo katika nchi imekuwa ndogo hivyo basi tutaangaza sekta baadhi ya njia za mabadiliko ili kuleta mabadiliko chanya.

Elimu na utamaduni
hivi sasa sekta hii imekuwa na matatizo mengi katika kuandaa watendaji wazuri wenye maadili ya hofu ya Mwenyezi mungu na Mtanzania, hivyo basi kuwepo na uwajibikaji katika ufundishaji somo la maadili na kuandaliwa kwake mtaala wahusishwe viongozi wa dini kuanzia mashuleni na vyuoni sambamba na kuwepo na waalimu wa dini waajiliwe na serikali.Serikali iweke mafunzo ya stadi za maisha mfano kilimo,ufundi, udereva n.k. kwanzia mashuleni mpaka vyuo vikuu vyote iwepo kozi moja ambayo atasoma kwaajili ya kumsaidia atakapo hitimu pia awe na ujuzi.( mfano fundi, dereva, n.k)

sekta ya uvuvi
Nchi yetu imekuwa na bahari, maziwa pamoja na mito. Sekta ya uvuvi inachangia ukuaji wa uchumi wa nchi, hivyo basi mabadiliko yanatakiwa kuwepo kwa kila mkoa kuwepo na mabwawa ya kuanzia ya Samaki 100 ambayo kila miezi 6 tutavuna Samaki kuuza katika makampuni. Hii inatakiwa serikali ķupitia Tantrade kutafuta masoko nje ya nchi kwa kasi hii ongezeko la pato la taifa litaimarika ukijumrisha na mbinu nyingine za awali ambazo serikali ilikuwa inatumia.

Sekta ya mifugo
Nchi yetu tuna wanyama kama mbuzi, ngombe wa maziws kisasa na nyama, kondoo, kuku n.k
Serikali inatakiwa kuwa na aina 5 tofauti za wanyama kila mkoa yani wastani 1000, maeneo yatengwe na wakala wa serikali wa mauzo awepo kwaajili ya ufanisi wa kazi hizo njia hii itasaidia upatikanaji wa viwanda na kutengeneza bidhaa zinazotokana na wanyama na pia uchumi utaongezeka.

sekta ya kilimo
hii ni sehemu nyeti ambayo inaongeza kwa haraka pato la taifa na bado nchini kwetu tuna maeneo yaliyokuwa wazi kwaajili ya kufanya kilimo. Serikali itenge kila mkoa hekta 300 kwaajili ya kilimo cha mahindi mtama, mpunga, kokoa,korosho n.k na kila mwaka itakuwa inaongezwa eneo kulingana na uwajibikaji. Kwa kuwatumia wataalum wetu wa kilimo chuo cha sua ili jambo ni jepesi na ongezeko la uchumi litakuwa kubwa.

Sekta ya Madini
Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa kuwa na madini mengi kwa aina tofauti tofauti kwa robo nne ya mwaka uzalishaji wa dhahabu ni kg 14 2023 kwa mujibu wa wizara husika chanzo kutoka taasisi ya Takwimu. Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zina dhahabu nyinyi.
Hiyo basi serikali kwa kutumia wataalamu wa madini kila mkoa kuwepo na eneo la uchimbaji la serikali na pia kununua kutoka kwa wachimbaji wadogo wadogo na biashara ya madini mnada wa serikali ufanyike kila baada ya miezi 3 tukiwa na Tani 5 au zaidi. Na madini kama tanzanite na mengine serikali iweke wastani wa Tani 5 na kufanya mnada. Bajeti ya nchi inaweza kutoka hapo kwenye sekta ya madini tu. Lazima tuwe makini kwenye sekta hii tunapigwa sana na uzalendo umekuwa mdogo maeneo yapo mengi yenye dhahabu nchini na uchumi wa nchi ndani ya miaka 5 ya mwanzo bajeti yake iandaliwe kutoka katika sekta hii.

Sekta ya Uchumi mipango na Fedha
hii sekta ni muhimu sana katika ukuaji na maendeleo ya nchi yetu. Lazima kuwepo na watu makini ambao watawezeshwa na wafanye kazi kwa uzalendo ili kuleta maendeleo yenye tija kwa Taifa.
Tunapozungumzia mipango ya Taifa lazima kuwepo na jopo maalum kwanzia ngazi ya kata mpaka taifa.
Pia usimamizi wa fedha kuhusu huduma zote lazima ziwe katika mpangilio unaofanana ili kudhibiti matumizi na mapato ya Taifa.

Kuna swala la wakwepa kodi lazima zitumike njia za kutambua bidhaa za watu pindi zinapoingia nchini kwa kuwepo na code namba maalum ya bidhaa hata zikiwa zimezagaa mitaani kama Mali haijalipiwa kodi system inasema ni nina kutokana na kuwepo na code namba ya biashara.

Miradi yote haiwezi kupiga hatua bila ya usimamizi mzuri lazima serikali kupitia kitengo cha Financial intelligence unit itoe ajira kwanzia ngazi ya kata mpaka Taifa na kila mradi wa serikali wawepo na mamlaka nyingine za kudhibiti ubadhilifu na wapewe nafasi ya kuingia kwenye akaunt za watendaji kila mara kujua miamala yako, hali hii itasaidia kutokuwepo na mwanya wa upotevu wa fedha za umma. Wananchi wapewe maeneo na serikali ya kufanya shughuli za kiuchumi na serikali ndio awe mnunuzi au mwekezaji ambaye anatoa vitendea kazi alafu atachukua Mali itakayopatikana.

Hitimisho
Kama miongozo mbali mbali itatolewa na wataalamu kwa kutumia hii fikra yangu ndogo tija itapatika na kila baada ya miaka 5 tutakuwa na kitu kipya cha kufanya cha maendeleo.
Ewe Mwenyezi Mungu ibariki Nchi yangu
 
Upvote 2
Ndani ya miaka 5 hadi 15 na kuendelea Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itakuwa ni miongoni mwa nchi ambazo zitakuwa zinatumia rasilimali zake 100% kwaajili ya makadilio ya bajeti ya nchi
Ebhana eeeeh! Hii ni 'move' ya kibabe sana. Sema duuuuh! Tunasikia hadi Marekani inadaiwa je na sie tutaweza kweli kuwa na uchumi wa 100% bila madeni?

Hii inatakiwa serikali ķupitia Tantrade kutafuta masoko nje ya nchi kwa kasi hii ongezeko la pato la taifa litaimarika ukijumrisha na mbinu nyingine za awali ambazo serikali ilikuwa inatumia.
Pointi nzuri sana hii, tunataka masoko yanayolipa vizuri ilo kusisimua uwekezaji na uzalishaji zaidi.

Nchi yetu tuna wanyama kama mbuzi, ngombe wa maziws kisasa na nyama, kondoo, kuku n.k
Serikali inatakiwa kuwa na aina 5 tofauti za wanyama kila mkoa yani wastani 1000, maeneo yatengwe na wakala wa serikali wa mauzo awepo kwaajili ya ufanisi wa kazi hizo njia hii itasaidia upatikanaji wa viwanda na kutengeneza bidhaa zinazotokana na wanyama na pia uchumi utaongezeka.
Tupo pamoja, lazima tuongeze uzalishaji na kukuza masoko ya bidhaa zake mifugo. Nikisikiaga mtu anaongelea kuipunguza namshangaa sana na hoja zake muflisi.

kuandaliwa kwake mtaala wahusishwe viongozi wa dini kuanzia mashuleni na vyuoni sambamba na kuwepo na waalimu wa dini waajiliwe na serikali
Kwa hilo nashauri masomo yasiwe ya dini kama dini bali Falsafa ya Imani zote. Kuhusisha wote wanadini, watamaduni, wafalsafa na wasionadini katika kujenga falsafa kamilifu ya maisha ya Taifa letu itapendeza. Au unaonaje?

miongozo mbali mbali itatolewa na wataalamu kwa kutumia hii fikra yangu ndogo tija itapatika na kila baada ya miaka 5 tutakuwa na kitu kipya cha kufanya cha maendeleo.
Ewe Mwenyezi Mungu ibariki Nchi yangu
Ahsanye sana
 
Ebhana eeeeh! Hii ni 'move' ya kibabe sana. Sema duuuuh! Tunasikia hadi Marekani inadaiwa je na sie tutaweza kweli kuwa na uchumi wa 100% bila madeni?
Tuanze bro maana serikali yetu kama kila mmoja akiwa mzalendo wa kweli inawezekana. Tuna madini ambayo dunia nzima inatuangalia sie kama nchi peke na tuna utalii wa kipekee pia why tusiweze.
Tupo pamoja, lazima tuongeze uzalishaji na kukuza masoko ya bidhaa zake mifugo. Nikisikiaga mtu anaongelea kuipunguza namshangaa sana na hoja zake muflisi.
Leo wizara husika inatakiwa kutoa takwimu za mifugo sambamba na pesa ambazo zinatolewa kila mkoa kwaajili ya maķundi maaluum mimi kwa maoni yangu wapewe shaba la mifugo itasaidia uzalishaji na pia masoko yatafutwe. Mfano visiwa vya comoro mbuzi anaeshimiwa sana basi tutengeneze connection za kibiashara na nchi nyingi tu mbuzi nyama yake ni inauzika sana. Sasa tunashinďwa nini au tuwaachie hizo biashara wafanye viongozi wastaafu why???
 
Tuanze bro maana serikali yetu kama kila mmoja akiwa mzalendo wa kweli inawezekana. Tuna madini ambayo dunia nzima inatuangalia sie kama nchi peke na tuna utalii wa kipekee pia why tusiweze.

Leo wizara husika inatakiwa kutoa takwimu za mifugo sambamba na pesa ambazo zinatolewa kila mkoa kwaajili ya maķundi maaluum mimi kwa maoni yangu wapewe shaba la mifugo itasaidia uzalishaji na pia masoko yatafutwe. Mfano visiwa vya comoro mbuzi anaeshimiwa sana basi tutengeneze connection za kibiashara na nchi nyingi tu mbuzi nyama yake ni inauzika sana. Sasa tunashinďwa nini au tuwaachie hizo biashara wafanye viongozi wastaafu why???
TUtafika tu, tutafika
 
Back
Top Bottom