Tanzania Nchi Yenye uwezo mkubwa ktk Usalama wa Taifa

Tanzania Nchi Yenye uwezo mkubwa ktk Usalama wa Taifa

Status
Not open for further replies.

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Nina andika hii mada nikiwa nafuraha kubwa. Vile hili taifa linauwezo mkubwa ktk idara zake za usalama wa hili taifa. Huku nikiwaonya wale wanafikiri wanaweza kununua taifa hili wajuwe kuwa siku watakapoweza hilo, basi taifa hili litakuwa limekuwa vipande vipande.

Nijambo lakushangaza kuwaona watu wanaranda randa huku nakule wakifikiri eti wanaweza kuitia serikali ya J. K mfukoni. Nikukosa akili nakuwa na uwezo mdogo kufikiri.

Watanzania napenda kuwahakikishia mwaka 2015 mtajuwa kuwa hata baada baba wa taifa hili kutuacha bado ulinz,umoja na usalama wa taifa hili ni moja ya ajenda kuu pindi mtu awaye yeyote anae kasimiwa madaraka makubwa ktk taifa hili anakaa pale ikulu. Napenda watanzania mjuwe majeshi yote yaulinzi na usalama, pamoja na idara nyeti za usalama wa taifa hili wapo pamoja na Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha hakuna kiroboto ama kunguni ama sisimiz au mchwa analiharibu taifa hili.

Serikali yetu imejipanga kwa mipango ya muda mrefu na muda mfupi kuhakikisha hakuna makosa yatatoke. Hili ni taifa uru na hakuna mtu awaye yeyote ataweza kutumia uhuru tulio nao kuleta ujinga ujinga wake. Ndugu watanzania yatupasa kutubu kwavile some time tunamtukana even our Nation president eti dhaifu? Eti kisa mawaziri hawakai muda mrefu, Jaman do we know taarifa anazipata ktk idara njeti za taifa hili? Je tunajuwa anawatu wanao mshauri kutokana na taarifa wanapata toka ktk idara nyeti za taifa letu? If so kwanini tusione kuwa huyu ndie the best president we ever have? Huu ni wakati wakujuwa hili taifa ni taifa lenye nguvu na uwezo mkubwa ktk kufanya mambo yake na kama mnataka juwa udhaifu wa bwana mkubwa subiri amalize Muda wake ndipo tuseme.

Kwa upande wangu nimejawa nafuraha kubwa maana najuwa mzee wangu na rais wangu J. K anafanya kazi ngumu ambayo haikuwah kufanywa na rais awaye yoyote, we need to pray 4him maana kutengeneza njia yakumpata mtu safi kwenda ikulu sio kaz rahisi. Wengi watamchukia ila baada yake urais kwa watu mafisadi ndio mwisho. Na kwa taarifa yako hata mafisadi wanajuwa hilo lakini yeye anasonga mbele.

Aman ya taifa hili ipo mikono mwako na kwangu, ila nilazima ujuwe ulipo zaliwa uli ikuta aman, ikimanisha wapo watu wanalilinda hili taifa usiku na mchana hvyo hakuna mwanachama,kiongoz ama mtu mwenye pesa anaweza vuruga aman la taifa hili.

Ndugu zangu tutulie na tuone haya nimeyasema. Maana wahenga walisema lisemwalo lipo, nakama halipo tulingoje maana laja. Thank u
 
wewe kichekesho sana, ulinzi gani unauongelea wa kuhakikisha CCM wanabaki madarakani ama ulinzi gani? hivi hawa wachina wanaogawana tembo wetu inakuwaje? hivi akina Dr.Mvungi, Ulimboka, and of that type and incidences huo ulinzi unakuwaje? hizo bei za umeme zinavyopanda, nadhani ungekaa kimya tu - wananchi tunaumia sana, usifanye utani please
 
Hawa ndiyo huwa wakilewa unawakuta wanaimba barabarani huku anayumba, hafu bahati mbaya kaamka na hangover akajikuta yale ambayo huwa anayaimba anayaandika JF.

Au aliarikwa kwenye harusi ya mtoto wa mwenye Kaya akajikuta amekula na kuvimbiwa toka juzi hivyo leo ndiyo amepata unafuu.
Naomba nikufahamishe ndugu Usalama wa taifa siyo kazi yao kumlinda Rais au kuamua nani awe rais kazi yao ni kulinda maslahi ya nchi hata akija Rais anamiraba 80 lakini anatakiwa kuongoza kwa kufuata misingi ya nchi inavyotaka nadhani umeniewa. Kijana usiwe unakurupuka tu
 
^^
Ni wazo jema lakini Asemae niko macho, niko macho ajihadhari asiangukiwe na mti
^^
 
Mbona hueleweki,kwani yeye alipoingia alikuta taifa haliko salama?na pia mbona hujajitambulisha,kwani wewe ni afisa habari wa vyombo vya usalama wa nchi hii?
 
Kiazi TumainiEl
===>Unawajua walio WATESA HAWA ?au wameshakamatwa?
1.Ulimboka
2.Kubenea
3.Kibanda
4.Dk Senkondo Mvungi?
===>Ukinipa majibu yake basi nitaamini unachosema,ila kama ni intelijensia ya mikutano ya cdm pia nitakuelewa.
 
Uliye andika huu uzi ungekua karibu ningekunasa kibao mpaka ujikojolee;Huna adabu kabisa na uchungu wa hili taifa na mali zetu;Mijitu imelala alafu unasema kuna usalama wa taifa kweli!;Kama upo mbona wameomba raia washirikishwe kwenye ulinzi?.


Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom