Tanzania ndio chuo Cha mafunzo Cha matibabu ya moyo Africa

"Tanzania ndio chuo...." ungeijua sekta ya afya ya Afrika Kusini ambako ndiko Waziri Mkuu wako mstaafu amelazwa na DG mstaafu wa Usalama wa Taifa alifia usingeandika hivi.
Bado hatujagusa Morocco, Egypt na Nigeria.
Labda wanakwenda nje kwa sababu nyinginezo na siyo moyo
 
"Tanzania ndio chuo...." ungeijua sekta ya afya ya Afrika Kusini ambako ndiko Waziri Mkuu wako mstaafu amelazwa na DG mstaafu wa Usalama wa Taifa alifia usingeandika hivi.
Bado hatujagusa Morocco, Egypt na Nigeria.
Mkuu, onyesha nchi mbili au tatu za Africa zilizoingia mikataba ya Serikali kwa serikali Ili kuwahudimia raia wao na kutoa mafunzo kwa nchi zao Kama zilivyofanya nchi zilizotuzunguka

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Nigeria ndio nini? Buhari (bokohari) hutibiwa Uingereza; hana imani kabisa na hospitali za Nigeria🤣
 
Tanzania ina huduma za afya kuzidi Nigeria?
Buhari kutibiwa Uingereza sio shida, au unaona UK ni level sawa kiafya na nchi yeyote Afrika hapa. Angeenda kutibiwa Chad Republic ungekuwa na hoja
 
Mkuu, onyesha nchi mbili au tatu za Africa zilizoingia mikataba ya Serikali kwa serikali Ili kuwahudimia raia wao na kutoa mafunzo kwa nchi zao Kama zilivyofanya nchi zilizotuzunguka

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
Kusaini mikataba na nchi mbili maskini sio kuwa chuo Afrika. Hao ambao hawajasaini wakija watatibiwa vilevile wakiwa na vigezo.

Tittle ya uzi inatia chumvi habari
 
Tanzania ina huduma za afya kuzidi Nigeria?
Buhari kutibiwa Uingereza sio shida, au unaona UK ni level sawa kiafya na nchi yeyote Afrika hapa. Angeenda kutibiwa Chad Republic ungekuwa na hoja
Weka ushahidi Kama Nigeria Kuna Hospitali yenye viwango vya JKCI, kwa idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa 1)Cardiac operation kwa mwaka, 2) Success rate, 3)Number of foreign countries which send their patients, 4) Modern Equipments

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Kusaini mikataba na nchi mbili maskini sio kuwa chuo Afrika. Hao ambao hawajasaini wakija watatibiwa vilevile wakiwa na vigezo.

Tittle ya uzi inatia chumvi habari
Sasa Kama huna mkataba na nchi yoyote ya Afrika kufundisha raia wake, na Kuna nchi yenye mikataba na nchi kadhaa za Afrika kufundisha raia zao, ni nchi ipi onayostahili kuitwa ni chuo Cha kufundisha African countries?, Kichwa Cha habari ni kuhusu chuo Cha mafunzo

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Weka ushahidi Kama Nigeria Kuna Hospitali yenye viwango vya JKCI, kwa idadi ya wagonjwa wanaofanyiwa 1)Cardiac operation kwa mwaka, 2) Success rate, 3)Number of foreign countries which send their patients, 4) Modern Equipments

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
Hiyo ni kazi ngumu kidogo na si lazima iwepo institution moja inayofanya kazi kubwa ukizingatia wako zaidi ya 210 million. Wako na cardiothoracic surgeons 75 sijui sisi tunao wangapi.

JKCI ina uwezo mkubwa na inafanya kazi nzuri, ila sio ukisifia kitu uzidishe
 
Sasa Kama huna mkataba na nchi yoyote ya Afrika kufundisha raia wake, na Kuna nchi yenye mikataba na nchi kadhaa za Afrika kufundisha raia zao, ni nchi ipi onayostahili kuitwa ni chuo Cha kufundisha African countries?, Kichwa Cha habari ni kuhusu chuo Cha mafunzo

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
Wenye sekta yao wakikusikia watakutandika makofi. South Africa ndio nchi ya kwanza duniani kufanya human to human heart transplant ilikuwa ni mwaka 1967 kipindi wazee wetu wako busy na Azimio la Arusha.

Tangu 1967 hadi leo 2023 Tanzania haijawahi fanya hiyo operation uko hapa unaongea tu kisa wanasiasa wamesema. Eti Tanzania inaizidi South Africa

Vitu wamefanya 1967 sisi bado, umekalia kwenye mikataba😂
 
Wenye sekta yao wakikusikia watakutandika makofi. South Africa ndio nchi ya kwanza duniani kufanya human to human heart transplant ilikuwa ni mwaka 1967 kipindi wazee wetu wako busy na Azimio la Arusha.

Tangu 1967 hadi leo 2023 Tanzania haijawahi fanya hiyo operation uko hapa unaongea tu kisa wanasiasa wamesema. Eti Tanzania inaizidi South Africa

Vitu wamefanya 1967 sisi bado, umekalia kwenye mikataba[emoji23]
Mkuu tuliza akili kidogo, hatujazungumzia kufanya operation, tumezumgumzia chuo Cha kufundisha nchi za Africa, hatuzungumzii uwezo wa kufanya operation kubwa.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu tuliza akili kidogo, hatujazungumzia kufanya operation, tumezumgumzia chuo Cha kufundisha nchi za Africa, hatuzungumzii uwezo wa kufanya operation kubwa.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
Kufundisha nchi mbili maskini za Afrika sio kitu cha ajabu. Wiki jana hujaona wanafunzi wa Tanzania wanatoka Sudan walipokuwa wanasoma kabla ya machafuko. Kwahiyo tuseme vile vyuo vya Sudan ambavyo havina hadhi yoyote ya kuzidi vyuo vyetu hapa nchini vinagundisha nchi za Afrika?

Hiyo si ni kama exchange program. Mnafanya hiki nao wanafanya kile, kwenye bandari hao tunawasaidia na hatuwezi sema "Tanzania ndio bandari ya Afrika" wakati kuna nchi zaidi ya 10 zenye bandari na wala bandari yetu haipo top 10 ya zinazobeba mizigo mingi.

Misifa itatufikisha wapi.
 
Ninapata wasiwasi na uwezo wako wa akili, samahani Kama nimekukwaza mkuu wangu. Niambie ni lini Tanzania iliingia mkataba wa serikali kwa serikali na Sudan Ili kufundisha wanafunzi wa Tanzania?.

Wafanyabiashara wa Kenya kwa muda mrefu walikua wakija kununua mbolea Tanzania, lakini hapakua na makubaliano rasmi kati ya serikali ya Tanzania kuiuzia Kenya mbolea, lakini juzi waziri wa kilimo alikuja rasmi Ili kuingia mkataba wa mauziano ya mbolea, kwanini unadhali walikuja kuingia mikataba rasmi wakati tayari wafanyabiashara wa Kenya kwa miaka mingi walikua wanaendelea kununua mbolea toka Tanzania?

Back
Top Bottom