Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kuita uchaguzi wa aina hii ni wa 'HURU NA HAKI'. Dunia nzima inaishangaa Tanzania, mbaya zaidi ni pale inapojinasibu huko duniani kote kwamba ni nchi ya kidemokrasia! Hii ni AIBU kubwa sana! Nahisi dunia nzima inashangaa na kuhoji kama watanzania ni watu wenye akili timamu au vinginevyo ni watu wenye IQ ndogo sana au kuna pahala akili za watanzania hazipo sawa.
Hii ni sawa na kusema mchezo wa mpira wa miguu kati ya Lesotho na Tanzania alafu kuanzia mashabiki, uwanja, refa, linesmen, match commissioner nk. Vinawekwa na kusimamiwa na Tanzania then utarajie Lesotho ishinde! Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kusema huo ni ushindani wa haki.
CCM imenufauka mno kwa miaka mingi kutokana na mfumo huu mbovu. Mbaya zaidi imetumia mfumo huu mbovu kujijenga na kujinufaisha mno kulinganisha na vyama vingine vya upinzani. Ni sawa na timu ambayo imeshinda makombe na fedha nyingi kwa njia hizo zisizo za kihalali kisha kwa miaka mingi hiyo ikatumia fedha hizo hizo kujipa nguvu zaidi kuendelea kutawala kwa njia zisizo halali.
Dunia inashangaa, Je, ni kwamba watanzania hawaoni jambo hili? Wamerogwa? Au ukosefu wa elimu? Umasikini?
Uchaguzi si kwa ajili ya ubunge na madiwani tu, ambapo kwa miaka mingi CCM imetumia njia ya kukubali ushindi kwa baadhi ya majimbo kwa vyama vya upinzàni ili kuuhadaa umma juu ya mfumo huu wa uchaguzi ambao si wa haki na huru, Na kwa bahati mbaya vyama vya upinzani vikishapata viti kadhaa bungeni vinasahau kwamba CCM kamwe hawawezi na hawako tayari kuachia serikali kuu kwa chama cha upinzani!
Je, Huu ndiyo uchaguzi huru na wa haki? HAPANA, huu si uchaguzi wa huru na haki.
MUNGU IBARIKA AFRIKA, MUNGU IBARIKA TANZANIA.