Kuna mambo ya kujiuliza kuhusu mafanikio ya Kenya. Kwanza je katiba yao ndio bora? Katika maeneo yapi?
Ni ngumu sana kukupa mifano halisi kuhusu Kenya na katiba yao maana sijaifuatilia sana. Pia haiwezi kuwa ndiyo role model pekee ya katiba duniani hapa.
Hata hivyo, kama katiba ya Kenya inampa mwananchi uwezo na uhuru wa kuhoji uwajibikaji wa viongozi, kama katiba inatoa nafasi ya kuhoji matokeo ya uchaguzi, kama katiba inapunguza ulimmbikizaji wa madaraka kwa mtu au taasisi moja, kama katiba inaziba mianya ya rushwa na inaweza kushughulikia wala rushwa bila kujali nani yuko madarakani, then i will go for it.
Katiba mpya haiwezi kufanya kile ambacho wananchi hawajaandika. Kama katiba haikuandikwa ili kuzuia upungufu wa ardhi, haiwezi kufanya hiyo kazi.
At least katiba inayoendana na wakati inafanya wananchi waweze kudhibiti mambo badala ya mtu mmoja au kikundi kidogo kufanya hivyo. Ikitokea mtu mzuri amemaliza muhula wake madarakani halafu likaingia genge la wala rushwa, wakabila, wabaguzi na wazembe halafu katiba haiwezi kuwafunga break, basi ujue itakula kwetu
Katiba bora ni ile inayotoa ufumbuzi wa matatizo ya wananchi wa kawaida, hayo uliyoyataja ya kuhoji na mengineyo ni mambo ya kisiasa zaidi, matatizo makubwa yanayoikabili Kenya hayajawahi kuwa ni kushindwa kuhoji matokeo ya uchaguzi, wala sio kulimbikiza madaraka, wala siyo hayo mengine uliyosema, matatizo makubwa ya wananchi wa Kenya ni ukabila, rushwa, kukosekana kwa usalama, kutokuwepo kwa usawa wa kipato kati ya matajiri na masikini, ardhi kumilikiwa na wachache matajiri, na ukosefu wa ajira, yale ya kuhoji na mengine uliyosema, ni kipaumbele cha wanasiasa lakini sio wananchi wa kawaida.
Hakuna katiba yoyote hapa Africa inayoruhusu rushwa, ukabila,, kukosekana kwa usalama, ukosefu wa ajira au kufagilia kuwepo kwa tabaka la matajiri na masikini, katiba zote zinakataza mambo haya ambayo ndiyo vipaumbele vya wananchi wa kawaida, kinachokosekana ni uongozi bora, Kenya ni mfano mzuri sana, walililia sana katiba mpya wakidhani katiba ndiyo itakayopita maofisini kugundua vitendo vya rushwa au ukabila na kuvizuia, kumbe watu ndiyo muhimu zaidi kulikokatiba, kama huna viongozi bora hata uwe na katiba ya namna gani hakuna litakalofanyika
Leo hii Magufuli ameweza kupambana na rushwa, uzembe maofisini, kupunguza gap la wenye nacho na wasionacho, na kushughulikia yale mambo ya msingi kwa wananchi wa chini kuliko Uhuru Kenyatta ambaye anatumia katiba mpya.
Hakuna katiba mpya itakayoshinda Biblia na msahafau, leo niambie ni mangapi yaliyosemwa kwenye vitabu hivyo tunayatekeleza?, hatutekelezi kwa sababu hakuna mtu wa kusimamia utekelezaji wake, kama tumeshindwa kufuata maagizo ya dini, vipi tutafuata katiba mpya, tusiwe tunawasikiliza wanasiasa kwasababu utaona wanayopigia kelele ni kuwa na uhuru wa kuhoji matokeo ya urahisi mahakamani, kwa urais ni muhimu kuliko hayo yote niliyokutajia, muhimu ni kumpata kiongozi bora atakayesimamia katiba iliyopo kwanza, aifuate kama ilivyo, tukishaimaliza hii iliyopo tukiona inatuzuia kupanda maendeleo ya watu, sio maendeleo ya wanasiasa ndiyo tufikirie vinginevyo.