Tanzania needs these kinds of roads currently!

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643


barabara za jinsi hii zitasaidia sana hasa kwa miji kama dar es salaam, mwanza, arusha, tanga na mbeya!

sijui kama serikali inaweza kuafford kitu kama hiki!

naomba kama magufuli yumo humu jf apitie kitu hiki!
 


barabara za jinsi hii zitasaidia sana hasa kwa miji kama dar es salaam, mwanza, arusha, tanga na mbeya!

sijui kama serikali inaweza kuafford kitu kama hiki!

naomba kama magufuli yumo humu jf apitie kitu hiki!

Mfano wa barabara zinazotakiwa hapa Tanzania.

Yes..!! Tunaweza kujenga hizi barabara kwa kutumia utajiri wa nchi yetu..!!
 

Attachments

  • bondeni.jpg
    113.4 KB · Views: 203
  • barabara za juu.jpg
    106.4 KB · Views: 208
  • south01.jpg
    31.2 KB · Views: 175
  • south02.jpg
    117.9 KB · Views: 174
Mfano wa barabara zinazotakiwa hapa Tanzania.

Yes..!! Tunaweza kujenga hizi barabara kwa kutumia utajiri wa nchi yetu..!!

ila ndugu, hawa madereva wetu vibomu wataweza kweli kufuata sheria za hizi barabara?
 
Hii inaweza kuwa Morogoro, mwaka 2020.

Angalieni njia za reli kwenye picha kushoto.

 
Kujenga fly over au free way kunahitaji eneo kubwa sana.

Tatizo hapa nchini watu wa mipango miji ni rushwa tupu. Watu wamepewa vibali vya kujenga magorofa hadi kwenye kingo za barabara.

Changamoto itakayokuja indapo tutajenga barabara kama hizo ni kuwa gharama ya kulipa fidia yaweza kuwa sawa au ikaizidi gharama ya kujenga barabara.

Majumba, mahoteli na masheli mengi sana itabidi yabomolewe.
 

Ni maamuzi tu kaka. Unafumba macho unatekeleza, mwanzoni wakati unatekeleza unaweza kubezwa, faida inakuja kujulikana baada ya miundombinu kukamilika. Angalau kwenye masterplan ingewekwa tu idea hiyo ya prototype kama ile ya mji wa Kigamboni basi tukawa na ndoto za implementation miaka ijayo, lakini hata mpango tu kwenye makaratasi sijaona wa barabara za juu. Basi hata zile grade interchange( under pass na overpass) kwenye makutano hasa pale Ubungo, Tazara nadhani na Magomeni nazo chapuo lake kimya!
 
Mhhh...Magufuli aone? ataona lakini afanye haya akiwa chini ya uongozi wa nan? huu tunaoujua? sahau.... hii takataka ya Morogoro road ... Imetumika maximum effort yani haielezeki.. nafikiri umeona kilichofanyika. sasa fikiria haya makubwa ni lini yatafikiriwa kufanyika.:frusty::crying::crying::crying:
 
Kilichopo Wala siyo kubomoa kila kitu ni kuangalia jinsi ya Kuboresha barabara tulizonazo na kuwa na traffic management inayoendana na mazingira usika . Siyo kila mji au sehemu zinaitaji flyover . Kunabaadhi ya sehemu kwa mfano kwenye suala la upanuzi wa miji mipya ndio unaweza kuweka mipango ya flyover na tunnel kwani gharama itakuwa ndogo uhitaji kufanya compensation kubwa. Mambo kama haya ni kuweka mipango mizuri ya miji ya baadae. Kuna miji Mingi tu Ulaya ambayo haina mabarabara makubwa ktk ya miji na bado wana manage traffic yao vizuri. Kingine ni kuweka njia mbadala ya kusafiri kama train overground and underground na sio kutegemea motorised traffic road. Uwezi kuwa na zero congestion lazima kwenye peak hour uwe na certain per centage which is allowable. Kwani hakuna nchi ambayo haina congestion. Ni kama inflation lazima iwepo lakini ambayo inakubalika .
 

Tatizo letu ni kuwa tumekariri mji lazima uwe Dar!!!! Tungeweza kujenga hizo barabara sehemu nyingine kabisa yenye ardhi ya kutosha na Dar ingejifia tartiiiibu ikiupa nafasi huo mji mpya!!!!!!
 
ila ndugu, hawa madereva wetu vibomu wataweza kweli kufuata sheria za hizi barabara?

Mkuu binafsi huwa naendesha kwenye hizo flyover nikiwa rsa pamoja na hizi za hapa nyumbani , kiufupi ni rahisi kufata sheria kwenye fly overs kuliko single lanes,simply hakuna gari inakatisha barabara mbele yako! Hao unaowaita vibomu wanaweza kuwa fit sana kuendesha kwenye barabara hizo kuliko unavyo wadhania!!!
 
nichagueni mimi kuwa Rais wa hii nchi muone
Nalog off
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…