Wakuu nilishangaa sana kuona waliopandishwa kizimbani si wahusika!!! Aliyepeleka mzigo kuupakia ni nani?? Na alishirikiana na nani katika Wizara?? Hawa ndiyo tunawataka!!! A tuseme hayo makampuni ya clearing and forwarding waliingizwa mkenge na kuandika kuwa mzigo ni wao?? Kama walifanya hivyo, ni kwamba kesi inawaangukiwa wao kama ambavyo vinara wa EPA wengi walitumia watu au makapuni mengine kujichotea pesa na wenye makampuni halisi wanakoma ubishi sasa hivi. Tusubiri tuone?? Watakuambia hakuna ushahidi wa kutosha kumpata mwenye mali na pia maafisa wa mali asili na utalii. Au tuseme ndiyo plan B ya finances of 2010?? baada ya ile ya EPA kuwaka moto!!!!???
Halafu pia kule TRA si wanakagua mzigo in and out?? Au huwa wanaamini kinachoandikwa na mteja wao tu?? Tuambiwe na kitengo cha Inspection hakifanyi kazi yake sawa sawa!!! Kama ni kesi basi vinara bado hawajafikishwa kwa pilato. Kama serikali haihusiki na iko serious tunataka tuone haki ikitendeka na si kutafuta dogs wa kufa nao!!!!