SoC04 Tanzania ni nchi nzuri lakini imejawa na Viongozi wazembe

SoC04 Tanzania ni nchi nzuri lakini imejawa na Viongozi wazembe

Tanzania Tuitakayo competition threads

SAMWELI OGOLA

New Member
Joined
May 23, 2024
Posts
2
Reaction score
2
Tanzania ni nchi nzuri sana, Amani, Uhuru na Utulivu ni wa kutosha, Ila ni nchi iliojawa na viongozi wazembe sana japo ni wasomi sana

Tumekua tukiamini sana katika Uwekezaji hasa kwa Raia na Taasisi za kigeni kuliko kuwekeza na kusimamia sisi wenyewe?

Serikali haifanyi Biashara ila inatoa huduma ila huduma nyingi mno ni mbovu sana yani utadhani ni Serikali ya kuadhibu watu wake kulingana na huduma inazotoa.

Napenda kuongelea sekta ya Usafiri na usafirishaji. Kumekuwa na changamoto kubwa sana hasa katika sekta hii, Wizara imeshindwa kuweka mazingira mazuri ya Magari kupaki na sehemu zilizotengwa kwa ajili ya pakingi bado ni changamoto kwasababu hazina mazingira rafiki kama vyoo na sehemu zenyewe hazijaboreshwa kabisa, zina mashimo na wizi sana. Mfano Shimo la Udongo, Sabasaba ni pachafu, mazingira mabovu sana ila ikija kwenye ada au gharama ya pakingi ni kuanzia 5,000/= adi 10,000/= kwa siku 1.

Pia ni maeneo yenye nafasi ndongo sana za kupaki na hazina utaratibu mzuri kabisa wa kupaki ambapo mtu akipaki gari nyuma ni changamoto sana kutoa Gari.

Hii ni kwasababu serikali haina usimamizi mzuri kabisa, inashindwa kuajiri wabunifu wazuri zikajengwa pakingi nzuri na zinazokidhi mahitaji ya Binadamu, na pia itatengeneza ajira ambazo zitakuwa rasmi nyingi na zile zisizo rasmi pia zitakuwa nyingi.

Pia Serikali ingeweka muda wa hasa gari kubwa kupaki Barabarani angalau dakika 15 tangu linaposhikwa na wahusika wasikimbilie kupiga tuu faini, kwasababu madereva wa magari makubwa wengine wameenda safari mwezi mzima yuko nje au mbali na familia zao sasa hata kusimama kidogo tuu kushusha mizigo anapigwa faini 300,000/=

Ni uonevu mkubwa na wizi Serikali, Wizara wabuni na kuweka mazingira mazuri kwa wasafirishaji, ila faini za 300,000/= ni wizi na uonevu mkubwa.
 
Upvote 1
Tumekua tukiamini sana katika Uwekezaji hasa kwa Raia na Taasisi za kigeni kuliko kuwekeza na kusimamia sisi wenyewe?
Huu si ni uzembe kabisa huu. Ni lazima tuchape kazi na kujifunza kujisimamia kisawasawa.

Pia Serikali ingeweka muda wa hasa gari kubwa kupaki Barabarani angalau dakika 15 tangu linaposhikwa na wahusika wasikimbilie kupiga tuu faini, kwasababu madereva wa magari makubwa wengine wameenda safari mwezi mzima yuko nje au mbali na familia zao sasa hata kusimama kidogo tuu kushusha mizigo anapigwa faini 300,000/=
Kwa hapa asee nitaomba watu wote wafuate sheria tulizojiwekea kwa haki maana ikiwa tutawahurumia wataanza kupaki mabarabarani na kuoelekea foleni ajali na hasira zaidi tu kwa ujumla
 
Back
Top Bottom