Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa kuna wanasiasa malaya, na akaongeza kuwa wanasiasa malaya wana bei. Ukiifikia bei yake, ananunulika.
Ukweli huu wa mwalimu unaishi mpaka leo. Tuna wanasiasa wachache sana wa itikadi, yaani wale ambao liwake jua au inyeshe huwezi kuwaondoa katika kile wanachokiamini. Lakini ukweli ni kwamba, Tanzania tuna wanasiasa wengi ambao kiuhalisia wanatafuta maisha kupitia siasa. Hawa ni kama wachezaji wa mpira. Wanatafuta riziki. Riziki kubwa ikiwa Azam, atahama toka Simba kwenda Azam. Na siku riziki ikiwa kubwa zaidi Yanga kuliko Azam, anaondoka Azam kwenda Yanga.
Mifano ya wanasiasa wa namna hiyo ni mingi. Lakini mfano wa karibuni, ni huu wa ndugu yetu Msigwa:
1) Msigwa akizungumzia uozo uliopo ndani ya CCM, alisema kuwa siku akiondoka CHADEMA, akaenda CCM, wananchi wa Iringa wachome moto nyumba na magari yake. Je, leo anaweza kuyarudia maneno hayo tena?
2) Msigwa aliwahi kusema kuwa matatizo yote ya nchi hii yamesababishwa na CCM, na hivyo haiwezekani CCM hiyo hiyo ikayatatua matatizo iliyoyasababisha yenyewe. Je, leo anaweza kuyanena hayo?
3) Msigwa aliwahi kutamka kuwa CCM walitaka kumnunua, na Ndugai alimfikishia ujumbe kuwa Rais Magufuli anamkaribisha Ikulu, na akikubali kuihama CHADEMA akaenda CCM, Magufuli ameahidi kumpa uwaziri. Lakini yeye Msigwa akadai ana msimamo, siyo mtu anayeweza kununuliwa hovyo hovyo kama ilivyofanyika kwa wengine. Je, anaweza kuyanena hayo tena leo? Au yeye umenunuliwa vizuri, siyo hovyo hovyo kama wenzake?
4) Hivi karibuni, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, aliwaambia kuwa, baada ya kuukosa uongozi ndani ya chama chake, kuna watu walikuwa wanasubiria atangaze kuhamia CCM. Akasema hilo halitaweza kutokea, kwani yeye hakuwepo CHADEMA kwa sababu ya cheo. Je, anaweza kuyasema hayo hata leo?
5) Msigwa anasema CHADEMA imekuwa SACCOS ya mtu mmoja, lakini hakuwahi kuyanena hayo miaka yote alipokuwa kiongozi wa CHADEMA. Au anataka tuamini kuwa yeye aliifanya Kanda ya Nyasa kuwa SACCOS yake binafsi, hivyo alivyoondolewa ameshangaa inakuwaje mwenye SACCOS kuondolewa?
NB. Lakini wenye macho ya kuona mbali, walikuwa na mashaka na Msigwa tangu pale viongozi wote wa CHADEMA walipowekwa jela, halafu yeye akatolewa kwa pesa iliyotajwa kuwa ilitolewa na Hayati Magufuli.
Ujumbe ni mmoja tu, nchi haiendi wanapopatarajia wananchi kwa sababu viongozi wengi wanatafuta uongozi ili kuyategemeza maisha yao
SAFARI YETU YA KUPATA MABADILIKO CHANYA, BADO NI NDEFU NA NGUMU, Japo hatutakiwi kukata tamaa.
Tukumbuke, kwa kila harakati, hawakosekani wasaliti, wanafiki, waongo na mamluki.
Hivi kweli kwa mtu yeyote anayechukia udikteta au rushwa, anaweza kutoka chama chochote cha upinzani, akaenda CCM?