SoC04 Tanzania niitakayo ithamini ubunifu wa ndani wa kuufanya rasilimali yenye manufaa zaidi

SoC04 Tanzania niitakayo ithamini ubunifu wa ndani wa kuufanya rasilimali yenye manufaa zaidi

Tanzania Tuitakayo competition threads

nasaris

New Member
Joined
Nov 25, 2019
Posts
1
Reaction score
0
Nitaanza na simulizi fupi ya wakati nikiwa kama darasa la tano ivi niliona kwenye gazeti moja kuhusiana na mwanajeshi aliyebuni genereta/injini inayotumia upepo,mwanajeshi huyo alisema alibuni injini hiyo wakati wa vita ya Tanzania na Uganda gari yake ilipoisha mafuta na kuibadili kuwa ya kutumia upepo.

Baada ya kusoma hiyo taarifa Hii ilininitengenezea wazo la kwanini serikali isiunde utaratibu wa kukuza ubunifu wa ndani na kuufanya rasilimali kubwa zaidi ya izi tulizo nazo, tuchukue tu mfano wa hiyo injini ya upepo vipi tungeanza kuzalisha magari ya aina hiyo na tukayauza yakiwa na brand ya nchi yetu maana yake tungetangaza jina la nchi na kikubwa zaidi tungepata pesa nyingi za kigeni na kukuza uchumi wetu kwa kasi kubwa kadri siku zinavyoenda na ubunifu mwingi kuongezeka.

Au angetengeneza hizo injini zikauzwa kwa bei ya kizawa kwenye maeneo yenye upepo mwingi (japo kwa makala yake alisema haiitaji upepo mwingi sana) ili kuwa chanzo mbadala cha nishati. Japo nilikuwa mdogo kiasi chake ila nilihuzunika sababu nihisi kwamba ujuzi wake usingetumika kwa manufaa ya taifa ili hali hata kam haukuwa ubunifu mkubwa kama inavyotakiwa ungeweza kutumika kuwa chanzo cha ubunifu mkubwa.Kumbuka ata kompyuta ya kwanza ilikuwa kubwa sana lakin ona leo.Apo ndipo ilipozaliwa sera kichwani mwangu ambayo kiufupi nishatafuta kuitolesera ya UNA NINI?

SERA YA "UNA NINI" NDIYO TANZANIA NIITAKAYO MIMI
Una nini ni nini? hili ni wazo langu lililoangazia kukuza ubunifu wa aina yoyote ile, nikiimaanisha katika kila ubunifu serikali iweke mkono wake kwani tuna wabunifu wengi sana kana kwamba tukisema tutumie hizo rasilimali akili walizonazo watu hakika ni zaidi mara mia ya hii migodi, vivutio vya utalii na kila kitu tulicho nacho,ni zaidi ya elimu tunayosoma ya uvumbuzi na akili za watu wengine.

Tanzania ni itakayo miaka 25 ijayo ni ile itayothamini ubinifu aa ndani na kuacha kutegemea tekinolojia kutoka nje,tukianza taratibu tukawa tayari kusimama miaka 20 ijayo tutaanza kuvuna matunda. Amna kitu kibaya kama kutegemea tekinolojia ya mwenzako kwenye dunia ya sasa iliyojaa vikwazo vya aina nyingi.

SERA IWEJE
Sera itaangazia ubunifu kama ifuatavyo:

1. Ubunifu binafsi
Hii itakuwa maalumu kwa wale waliovumbua vitu binafsi wa tofauti ambao haujawahi kuwepo au kama upo una kitu cha ziada zaidi kitachoonekana wazi na timu itayokuwa imeundwa kutafuta wabunifu.

2. Ubunifu wa taifa
Huu ni ubunifu utaoangazia lengo la taifa kulingana na uhitaji au mpango wa taifa,mfano kama tutataka kujitegemea kwa kuwa na satelaiti yetu na kila kitu kimtandao kitachofanyika ni kwamba kwrnye ubunifi aa taifa itatangazwa tendaa watakaukuja na wazo bora zaidi litapokelewa na kupewa nguvu na serikali kisha itaungana na idara ya tekinolojia ya anga tutatengeneza mfumo wetu sisi wenyewe.

UMUHIMU
1. Kuagiza tekinolojia inakufanya uwe mwagizaji(importer) zaidi ya muuzaji(exporter) kitu kinachoshusha uchumi zaidi.

2. Teknolojia yako inajulikana na kila mtu asa aliyeitengeneza hivyo kupunguza usalama binafsi mfano mzuri silaha.

3. Kuwa na tekinolojia yako kutakusaidia kwa kuwa endapo ikianza kuzalisha itazalisha ajira na kujenga uchumi na kuimarisha sarafu na kusaidia kuchimba hii rasilimali iliyosahaulika.

ITAKUAJE TUKIKUPUUZA
1. Itakuwa mmepuza rasilimali iliyoonyesha namna ya kupata rasilimali zenye thamani zaidi.

2. Kuendelea kuwa wategemezi wa kila kitu ata ambavyo tungeweza kuvibuni na kuvitengeneza wenyewe tuwaambie watu waje na mbegu salama ya mahindi ambayo ukipanda hekari moja utavuna gunia 100, ni ngumu kusoma ila kuna akili ipo sehemu inaweza fanya hili likawezekana sema hatupo tayari kuhiuisha(activate).

3. Kuendelea kubaki nyuma kwasababu hakuna mtu mjinga atayekupa ujuzi wake wote.

HITIMISHO
Pamoja na kuona faida zote za kutafuta ubunifu na kuupa nguvu ila pia hasara zipo kwasababu hakuna chenye faida kikakosa kuwa na hasara.

Itakuwa ni ujinga kupuza wazo hili kwa kigezo cha hasara zake labda iwe vinginevyo kwan ata wajasiria mali huchukua hatari(risk taker) ili wapate faida badala ya kucheza kwa uhakika (play safe) kukwrpa hasara uku faida ni kidogo sana na mda mwingine kuambulia hasara tu.

Nimezungumzia kila mwaka lakini kwenye uninifu wa taifa unaweza ukawa unafanyika kila baada ya miaka miwili au kivyovyote kikubwa tu tusiache haya madini yaliyopo kwanye akili za watu bila kuyatumia.

Hoja yangu kubwa si kushinda shindano ni kuona serikali imeliona ili wazo na kulifanyia kazi hii ni kwasababu hakika endapo litafanyiwa kazi kiundani bila kuleta siasa Tanzania ndan ya miaka si zaidi ya ishirini itakuwa hatua nyingine tofauti na itaigwa na nchi nyingi duniani.

Nimalize kwa kusema ndani ya akili zetu kuna kila tukitakacho ubunifu upewe kipaombele ili uweze kufanya vipaombele vingine viwe mbele kiukweli na siyo mbele kimzaa au kisiasa.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom