SoC04 Tanzania Niitakayo ni yenye vipaumbele hivi

SoC04 Tanzania Niitakayo ni yenye vipaumbele hivi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Posho City

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2012
Posts
648
Reaction score
418
Tanzania niiyakayo mimi ni ile yenye vipaumbele vya maeneo kadhaa na ntaichanganua kama ifuatavyo:

Elimu; eneo hili kwa Tanzania niitakayo linatakiwa kuwa na mikakati madhubuti na iwe na mambo haya...

Elimu ya ufundi iwe rasmi...shule za ufundi zilizopo zile 9 za serikali ziwe na miundombinu ya ufundi wa uhakika na wanafunzi wanaotoka zile shule wawe wameiva haswa kwenye fani zao...na serikali iwe na database ya kuwafatilia wakishahitimu ili kujua wapo wapi...wanafanya nn na wanachokifanya kina manufaa gani kwa taifa..

Lakini shule za vipaji maalum gazitakiwi kuwepo maana ni upotevu wa raslimali na ukitaka kujua hilo angalia database ya wahitimu wa shule hizi...ni wachache sana ambao wanalisaidia taifa kwa kusoma kwao shule hizi....kwa kuanzia hizi shule zote saba nitazigeuza ziwe shule za michezo zenye miundombinu yakinifu ya michezo..zitakuwa zinarecruit wanafunzi wanamichezo mbalimbali kwa umri wa under14...under...17 na under 20...kwa maana baadhi ya shule hizi zitakuwa za unde14 tu na wanaohitimu wanaenda kusoma hatua ya pili ya zile under 17 na akihitimu hapo anaenda zile za under 20...from there anakuwa amekuwa tyri kwenye mchezo husika na anaweza uzwa na kucheza popote
..Upande huu tukifanya hivi patatupatia mapato ya kiuchumi makubwa sana na kama nchi tutakuwa vizuri..

Kila mkoa tutakuwa na wiki ya ubunifu ya watu wasio na majina kabisa na itakuwa mara moja kwa mwaka...kwamba watanzania wasio na majina katika wiki ya ubinifu kila mmoja anakuwa na kitu chake alichobuni cha teknolojia ya aina yyte na wale watakoonekana kuwa vizuri kwa kila mkoa wanakutanishwa wanashindanishwq na tunapata the best top five kila mwaka...hawa mawazo yao ya kiteknolojia yanasimamiwa na kuboreshwa na serikali na yanaingizwa wenye wizara husika kuhusika kuendeleza nchi kiuchumi...

Tanzania niitakayo mimi makatibu wakuu wa wizara zote kama watendaji wa sekta muhimu kwa maana ya wizara watapatikana kwa mtindo wa usahili...zinatangazwa nafasi kwa watanzania wenye sifa kadhaa kwenye wizara husika na kila mmoja anakuja na mawazo yake kwa vitendo kulingana na uhalisia wa nchi...atakayeonekana kuwa vizuri ndiye anakuwa katibu mkuu wa wizara hiyo..

Mashuleni pia mfumo wa elimu yetu nitaubadilisha na nitahitaji kuwa na shule mia mbili nchi nzima za kuanzia ambazo hizi zitakuwa na multiple carriculum....maana naye nini shule hiyo hiyo inakuwa na madarasa ya michezo...ya muziki...ya biashara...ya masomo ya kawaida haya....ya fani mbalimbali pia..kwahiyo watoto wakija kidato cha kwanza hadi cha pili...wanasoma masomo yote kawaida ila wakishafika kidato cha tatu kila mmoja kwenye hizo shule ana uhuru wa kujiunga darasa alitakalo..

Haya yakifanyika baada ya miaka kumi tu kama nchi tutakuwa mbali sana.

Lakini huwezi kuwa na watu wenye kuzalisha yote hayo bila kuwa na miundombinu madhubuti kwenye afya...Tanzania niitakayo sekta ya afya kwanza lzma kila mtanzania halisi ambaye ni mtu mzima...serikali ihakikishe analipia bima ya afya ya kwake na ya familia yake....
Akishalipia kwa mwaka lzma kama nchi tuhakikishe tunakuwa na huduma za afya madhubuti kwa nchi nzima kuanzia ngazi ya mtaa/kijiji na huduma za afya ziwe na namba ya kitengo cha huduma kwa wateja cha dharura kama ilivyo kwa zimamoto...tanesco....nk
Mwananchi kupitia huduma hii awe na uwezo wa kujua huduma ya afya ya ngazi fulani inayopatikana karibia na mahali alipo.....na kila mwisho wa mwaka wa fedha....mapato ya bima ya afya yanachambuliwa matumizi yake...kiasi gani hakikutumika na kama nchi kupitia wawakilishi waamue kitumike kuboresha wapi na nini
 
Upvote 4
Mimi ninaitaka Tanzania ambayo viongozi wana huruma na rasilimali za nchi. Wawe waleta maendeleo ya kweli. Rasilimali za Nchi zifaidishe watanzania wote.
 
Back
Top Bottom