Tanzania pekee ndo kuna abiria wa aina 7

chavalla

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
451
Reaction score
354
_________________________________________________

Yupo abiria anayemtukana Konda ...lakini kumbe nauli ameacha nyumbani.

yupo aliyepitiwa na usingizi...huyu anapokurupuka hajielewi....utasikia shushaaaa bwege wee!..........anashushwa kambi ya jeshi!

Yupo mwingine msumbufu na mvivu halafu ana lawama....huyu anakaa mbali na mlango halafu usishangae akaomba msaada kwenye round about.

Yupo aliye makini na Safari..yeye anakwenda na Muda, huyu ukimpitisha kituo gari itajikuta Sumatra Head office.

Halafu Yule wa siti ya nyuma yeye hukoroma na tiketi mkononi ...huyu haigwi. ...maana mara nyingi hushukia kituo cha mwisho hata kama ni Makaburini.

Yupo asiyeelewa jina la kituo..amekariri panauzwa Mananasi Mengi, sasa akikuta Wameweka Matikiti basi ataenda na gari mpaka gereji.

Wa mwisho ni Staff...halipi nauli...huyu yeye hana safari maalum, ni kama anafanya utalii wa ndani, huyu hashuki hata kama ni trip ya Mkaa.

Ni yupi aliyetisha hapo..
 
Kuna wale wasio elewa kabisa wapi anaenda. Yani hapajui
Utasikia kila dakika hapa n wapi?
 
Lazma ujute kuzaliwa Yupo abiria anaye mtukana Konda ...lakini kumbe nauli ameacha nyumbani.
 
Huyo wa gari kulikuta Sumatra head office hahahah
 
Konda uwe unataja vituo bwana, sioni nje, aaaagh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…