Mimi ni Yanga na natambua ubingwa mwaka huu ni mgumu kutokana na ukweli kwamba timu yetu ni ya kawaida na hivyo haigopwi na wapinzani tunaokutana nao kama ilivyo kwa watani wetu Simba. Tusipokuwa makini hata kombe la shirikisho tutaishia kutolewa pia.
Tuwe tu wavumilivu msimu huu kama ilivyokuwa msimu uliopita. Ufanyike uchaguzi kama ulivyopangwa hiyo mei 5, wapatikane viongozi makini; usajili makini ufanyike mwisho wa msimu ili tuweze kurudi kwenye ubora wetu. Wachezaji wazee, wale wa kawaida wasio na tija kwa timu kama Yanga na wasiojituma wapewe mkono wa kwa heri na kwenda kutafuta maisha kwingine.