Tanzania Premier League, KMC Vs Yanga Uwanja wa Taifa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Ligi Kuu Tanzania bara TPL, kuendelea kutimua vumbi kwa wakati huu wa saa 19.00 usiku, ambapo KMC kutoka wilaya ya Kinondoni, Dar kuwakaribisha Yanga SC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

kipindi cha kwanza zimeanza huku timu zote zikianza kwa kasi.

10' Kutoka uwanja wa Taifa KMC 0-0 Yanga.

Yanga wanalisakama lango la KMC lakini washambuliaji wanashindwa kutumia vizuri nafasi zao

30' Bado milango ni migumu uwanja wa Taifa

KMC 0-0 Yanga.

Timu zimeshambuliana kwa zamu ambapo Yanga wamefika lango la KMC mara 11 dhidi ya mara 7 ya KMC

45 za kipindi cha kwanza zimekamilika matokeo bila kwa bila

Hakuna kona kwa Yanga SC wala upande wa KMC katika mchezo huu wa TPL.

Mpira umeanza kipindi cha pili, uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

55' Yanga wanakosa bao kwa shuti kali kugonga mwamba

60' Mchezaji wa KMC anakosa bao la wazi ndani ya 18 baada ya shuti lake kupaa juu ya lango.

80' KMC 0-0 Yanga SC uwanja wa Taifa.

87' Yanga wanapata faulo kuelekea lango la KMC

Gooooal gooooal 89' mchezaji Feisal Salum Toto anaipatia Yanga bao la kwanza baada ya free kick yake kwenda moja kwa moja wavuni.

Naaam mpira umekwisha uwanja wa Taifa ambapo Yanga wamefanikiwa kushinda mchezo huo kwa goli hilo moja dhidi ya KMC

KMC 0-1 Yanga

Ghazwat.....Asanteni sana

 
45' za mtanange kati ya KMC na Yanga umekamilika katika kipindi hiki cha kwanza

Ambapo timu zote zinakwenda mapumziko matokeo yakiwa KMC 0-0 Yanga
 
55' Gooo lah lah lah Yanga wanakosa bao kwa shuti kugonga mwamba wa lango
 
KMC inaonekana wako vizuri sana Yanga wanapata tabu sana
 
60' mchezaji wa KMC akiwa ndani ya 18 kupiga shuti na kupaa juu lango la Yanga
 
75' Tambwe anaingia. Kamusoko anakwenda kwenye benchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…