Tanzania Premier League 'TPL' Biashara United dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Karume Musoma

Tanzania Premier League 'TPL' Biashara United dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Karume Musoma

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania kuendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwanja wa Karume Mjini Musoma, ambapo Biashara United wakiwakaribisha Simba SC

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu kwa muda wote wa dakika tisini.

Biashara United, wanahitaji alama tatu ambazo ni muhimu kwao ili wajinasue katika mstari wa kushuka daraja.

Simba SC, wao kwa upande wao wanataka alama tatu ili waweze kuendelea na mbio zao za kutetea ubingwa..!

•••========•••

90' Mchezo umemalizika katika dimba la karume ambapo Simba SC wameweza kuifunga Biashara United mabao mawili bila majibu

Mabao yote yakiwekwa kimiani na John Bocco 34, 41[emoji460][emoji460]

Biashara United 0-2 Simba SC



IMG_20190427_152514_371.jpeg
IMG_20190427_152435_911.jpeg
 
Biashara wapange kipa mahiri wa kudaka mikwaju ya penati!
 
Kama leo Simba wakiwa 12 uwanjani na Refa wao. Itakuwa wanajibu mapigo ya utawala wa Malinzi. Maana tangu huyo jamaa alipokuwa Rais Yanga ilikuwa bingwa miaka yote hadi marefa toka Bukoba walikuwa wanathibitisha kuwa Faki hakuwa na kadi 3.
 
15' Biashara United 0-0 Simba SC milango bado migumu mpaka sasa..!
 
Ngapi ngapi hukoo jamani tunaomba updates
 
33' Gooooooaaaal. Goooooooaaaal John Bocco anaipatia Simba SC bao la kwanza kwa shuti kali la mguu wa kushoto..

...mpira ukigonga mwamba nakuingia wavuni na kumuacha golikipa akiruka bila mafanikio



Biashara United 0-1 Simba SC
 
41' Gooooooooaaaal....gooooooooaal goooooooal

John Bocco anaipatia Simba SC bao la pili kwa kichwa safi baada kupokea krosi ya Asante Kwasi

Biashara United 0-2 Simba SC
 
Back
Top Bottom