Tanzania Premier League 'TPL' JKT Tanzania Vs Simba SC Uwanja wa Mkwakwani

Tanzania Premier League 'TPL' JKT Tanzania Vs Simba SC Uwanja wa Mkwakwani

Yaani mwamuzi anaona aibu kutoa penati wachezaji wa simba wakishika ndani ya 18? Duh!
 
Tff na bodi ya ligi wamestushwa na mwenendo wa Simba wa kushinda magoli mengi imebidi wakae na uongozi wa simba na kuwaomba wapunguze idadi ya mabao na washambuliaji wao wasifunge hattrick kwani kwa sasa ligi haina mdhamini hivyo simba wakiendelea hivyo inawezekana ligi ikasimama kutokana na upungufu wa mipira ya kuchezea lakini habari nyingine ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa tff na bodi ya ligi imetishia kuwafungia waamuzi ambao wataruhusu wachezaji wa simba wafunge hattrick kwani wanaweza kusababisha ligi ikasimama
 
JKT wako vizuri sana, wakiongozwa na mkongwe Mwinyi Kazimoto.
 
Kabla mechi ya Jana walikuwa nafasi ya tano kwenye msimamo hii ni dhahir shahir wako vizuri

Lakini walikutana tu na mabingwa wa nchi
Sasa naanza kuiona Simba ikianza kucheza mpira niliokuwa nautaka.
Naanza kuiona kasi, nguvu na mikakati ya kupata magoli na stamina na pumzi.
Naomba radhi kwa maneno mabaya yoye niliyo msema kocha Uchebe.
Hakika Kocha wa Simba yuko vizuri na anamzidi sana Masudi Juma Irambona.
Naushukuru sana uongozi wa Simba SC kwa hii mikakata ya ukweli.
Thi si .....mba [emoji123]
 
Kwenye timu ya Taifa Stars,Simba ndio timu pekee yenye wachezaji 6,kwenye kila nafasi uwanjani.
Golikipa -Aishi Manula
Mabeki-Shomari Kapombe,Erasto Nyoni
Viungo-Jonas Mkude,Shiza Kichuya
Mshambuliaji-John Bocco.
Ushahidi wa timu iliyokamilika.
kwenye hao 6 wachezaji wa maana ni kapombe, Nyoni na mkude hao pimbi wengine hawana uwezo wanabebwa kishabiki
 
Huo ndo ukomavu wa soka mkuu wa kurudi kwa Kocha..

Tulipiga kelele sana kwanini akina Omog na Lechantre wanamnyoshea vidole Djuma, wengine tuligundua kuwa kuna tatizo mahala ndo maana alipoondolewa tulikubali.. Lakini shida ikabaki wale wasigundua kilichopo, tena wengine wakeenda mbali zaidi eti Aussems aondoke abaki Djuma

Yaani ni vichekesho kweli, kocha umemleta kwa gharama, ukamfanyia Interview na akina Msola pale Serena Hoteli akakidhi vigezo halafu aondoke kienyeji tu

Huyu kocha alifaulu ana kila kitu ambacho Simba walihitaji kwahivyo tuwe wavumilivu..SimbaNguvuMoja
Sasa naanza kuiona Simba ikianza kucheza mpira niliokuwa nautaka.
Naanza kuiona kasi, nguvu na mikakati ya kupata magoli na stamina na pumzi.
Naomba radhi kwa maneno mabaya yoye niliyo msema kocha Uchebe.
Hakika Kocha wa Simba yuko vizuri na anamzidi sana Masudi Juma Irambona.
Naushukuru sana uongozi wa Simba SC kwa hii mikakata ya ukweli.
Thi si .....mba [emoji123]
 
Kama Tambwe alivyofunga bao la mkono Simba Vs Yanga hivi hivi mwamuzi aliona aibu kukataa ndipo akakubali.
Yote ni yaleyale tu ingawa kwa mazingira ya Tambwe ni kama Goli la Maradona ni ngumu
Mwamuzi kung'amua lakini sio ule Upumbavu....
 
Kama yote yale yale..basi kubali kuwa waamuzi wanakosea duniani au toa goli moja ubao usomeki 0-1 kwako wewe

Ingawa kwa ujumla matokeo uwanjani yatabaki kama ilivyo.
Yote ni yaleyale tu ingawa kwa mazingira ya Tambwe ni kama Goli la Maradona ni ngumu
Mwamuzi kung'amua lakini sio ule Upumbavu....
 
Back
Top Bottom