Tanzania Premier League 'TPL' Ruvu Shooting Vs Simba SC, Uwanja wa Taifa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kivumbi cha ligi kuu Tanzania (TPL) kuendelea tena leo Oktoba 28, 2018 kwa mechi nne kupigwa katika viwanja tofauti huku gumzo likiwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam saa 1:00 usiku ambapo Ruvu Shooting itapambana na Simba SC.

Kuelekea kwenye mchezo huo, mkuu wa habari wa klabu ya Simba amesema hawadharau timu yoyote ambayo ipo Premier League kwa hivyo wamejiandaa kuwakabili vilivyo kuweza kushinda mchezo huo na kupata alama tatu muhimu, kama mabingwa wa nchi.

Kabla ya mchezo wa leo klabu ya Simba, Wekundu wa Msimbazi ilitoa ovyo kali kwa timu zinazoshiriki ligi kuu kwa kuwasambaratisha Alliance FC kwa mabao 5-1, ambapo Ruvu Shooting wakiwacharaza Singida United 3-0 mchezo uliopita, huku msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire akiwaambia Simba wajiandae kwa 'mpapaso Square'.

Aidha, kocha Hans Van Der Pluijm saa 10:00 jioni ataiongoza Azam FC dhidi ya timu yake ya zamani Singida United. Je nani kuondoka na alama tatu muhimu leo kwa timu zote? Usikose Ukaambiwa Kaa Nasiiii...!
••••••••======•••••••••••••

Vikosi vya mchezo wa leo Ruvu Shooting Vs Simba SC, tukianza na wenyeji ambao ni Ruvu Shooting;

Abdallah Rashid, Abdul Mpambika, Mau Bufu, Renatus Ambross, Temba Sued, Zuberi Dabi, Shaban Usala, Baraka Mtuwi, Said Dilunga, Fully Maganga, William Patrick.

Sub; Bidii Hussein, Yusuph Nguya, Hamis Kasanga, Chande Magoya, Adam Ibrahim, Khamis Mcha, Alinanuswe Martine.

Upande wa kikosi cha Simba SC katika mchezo wa leo;

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Juuko Murshid, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Cleoutus Chama, Meddie Kagere, John Bocco, Emmanuel Okwi.

Sub; Deogratias Munishi, Paul Bukaba, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Mohamed Ibrahim, Adam Salamba, Abdul Suleiman.

Naaaaaam mpira umeanza uwanja wa Taifa

00' Ruvu Shooting 0-0 Simba SC


07' Goooooooooaaaal gooooooaaal

Emmanuel Okwi anaipatia Simba bao la KWANZA baada ya kupokea pasi safi ya Kapombe

Ruvu Shooting 0-1 Simba SC

14' Bocco anapiga shuti la chini, lakini golikipa anadaka bila wasiwasi

Ruvu anashambulia lango la Simba, lakini mashambulizi hayaleti matunda

23' Meddie Kagereeeeeee gooooooaal..MK 14 anaandika bao la PILI baada ya kupigwa Kona

37' Ruvu wanafanya jaribio la mbali kwa kupiga shuti..Lakini mpira unatoka nje

Ruvu Shooting 0-2 Simba SC

45+2' Kuelekea kumalizika kwa kipindi cha kwanza. Naaaaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba wanatoka wakiwa mbele ya bao mbili dhidi ya Ruvu Shooting

Ruvu Shooting 0-2 Simba SC


Kipindi cha pili kimeanza..kwa kasi..Bocco anakosa bao dakika 46

Ruvu wanakwenda mbele. Lakini mabeki wa Simba wanakaa vizuri na kuzuia hatari zote.

53' Gooooooooooaaal Emmanuel Okwi anaipatia Simba bao la TATU kufuatia pasi ya Kapombee

Ruvu Shooting 0-3 Simba SC

77' Simba wanakwenda sasa kwake Kapombee Gooooooooooaaal, Emmanuel Okwi anaipatia Simba bao la NNE na kuhesabu Hat-Trick ya kwanza msimu huu

Ruvu Shooting 0-4 Simba SC

84' Adam Salamba anachukua nafasi ya Emmanuel Okwi aliyepata rabsha

Ruvu wanashindwa kutengeneza mashambulizi na kutoa nafasi kwa Simba dakika hizi za lala salama.

89' Dilunga anakwenda kwake Adam..Gooooooooooaaal Gooooooooooaaal..Adam Salamba anaifungia Simba bao la TANO kwa shuti kali nje ya 18

Ruvu Shooting 0-5 Simba SC

90+3

Wakati wowote mpira utamalizika uwanja wa Taifa

Naaaaaaam mpira umekwisha ambapo Simba wanaibuka na ushindi mnono wa mabao matano bila majibu dhidi ya Ruvu Shooting

Mabao ya Emmanuel Okwi 3, Meddie Kagere 1, Adam Salamba 1 akihitimisha kalamu ya mabao

Tumekuletea mtanange huu ni timu mzima ya JF

Asante sana...

Ghazwat
 

Attachments

  • FB_IMG_15407147957679326.jpeg
    63 KB · Views: 60
  • FB_IMG_15407147957679326.jpeg
    63 KB · Views: 55
Huyu dawa yake kama mauaji yaliyopita, kwavile anaongea sana

Na huenda akabadilisha usemo baada ya mchezo..SimbaNguvuMoja
Ombi langu kwa ndugu wa karibu wa Masau Bwire.. Wawe nae karibu sana baada ya mechi ya leo.. Maana kipigo tunachoenda kuwashushia vijana wake, kitakua na athari kubwa sana kwake.
 
Huyu dawa yake kama mauaji yaliyopita, kwavile anaongea sana

Na huenda akabadilisha usemo baada ya mchezo..SimbaNguvuMoja
Kutoka 'maktaba'..
Tangu msimu wa 2013/14, Mnyama Mkali Simba SC kakutana na Ruvu Shooting mara 8, ambapo Simba imeshinda michezo saba na wamelazimisha sare moja tu (Kwa kumbukumbu zangu, hii sare ilikua na utata mwingi saaana).

Sasa huyu Ndg. Bwire hii jeuri ya 'kusema sema' juu ya Mnyama, anaitoa wapi?? Au kutumwa huyu na wazee wa kutembeza bakuli??

Tulipanga tumpe kipigo kidogo tu, sasa kwa kua anatumika, tunaenda kumuadhibu yeye na aliyemtuma.
 
Yes...yes...endeleeni kumwaga madini wachambuzi kutoka timu Lunyasi..uwanja ni wenu huku tukimwambia Bwire ajiandae kisaikolojia.

Tutamfunga huku tukitoa burudani kama falsafa yetu..SimbaNguvuMoja
 
Unajitoa fahamu..Shooting inashinda, baada ya muda unagundua kuwa kumbe ni ndoto tu kushinda haiwezekani..Unakasirika Unakufa[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mechi 3 za Mwisho za Ruvu Shooting..
Mwadui 0-0 Ruvu Shooting
Kagera Sugar 0-0 Ruvu Shooting
Ruvu Shooting 3-0 Singida United

Mechi 3 za Mwisho za Simba SC..
Simba SC 2-1 African Lyon
Simba SC 3-0 Stand United
Simba SC 5-1 Alliance FC

Kwa hivi vitakwimu kidoogo, Masau Bwire haogopi kweli?? Na saa 1 ifike.
 
Hivi demigod unashangilia timu gani Premier League?

Hatukuoni kuna mwenzako Mwana Mtoka Pabaya kahamia Mbao FC akipoteza kumbukumbu za nyuma namna alivyonyanyaswa na Mbao FC[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Swala hana amani na Simba mbugani
 
Kwa takwimu hizi Masau bwire lazima ashikwe na tumbo na kuhara SIMBA ni tishio ni mwendo wa kung'ata tu [emoji75] [emoji75]
 
Hawa Ruvu wanautani kweli.. Yaani ndo wametuletea hawa wapambane na kina Chama, Okwi, Bocco, Wawa, Kapombe n.k??

Kwa kikosi hiki tulipanga Simba B nao leo wapashe pashe Taifa, ila kwa kua wameleta dharau.. Tunawashushia Full Mziki.
 
nyie simba leo lazima mshikwe mkia wenu, bungusiro fc
 

Attachments

Aisee wanasikitisha sana sasa hapo wanategemea wapate angalau sare mbele ya MNYAMA mwenye hasira kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…