Tanzania Premier Leaguer (TPL).... Ruvu Shooting wakiwakaribisha Young Africans uwanja wa Uhuru, Dar es salaam

Tanzania Premier Leaguer (TPL).... Ruvu Shooting wakiwakaribisha Young Africans uwanja wa Uhuru, Dar es salaam

Snipes

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2013
Posts
9,165
Reaction score
16,791
Ligi Kuu Bara inaendelea leo katika uwanja wa Uhuru, kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Yanga. Endapo klabu ya Yanga itaondoka na pointi tatu katika mechi ya leo, moja kwa moja Yanga itaenda kuongoza ligi kwa pointi 83 wakiwa wamebakisha mechi mbili kumaliza ligi, huku ikiiacha Simba kwa pointi moja nyuma wakati huo Simba ikiwa na michezo 5 mkononi.
LINE-UPS
FB_IMG_1557837163071.jpg


FULLTIME; Ruvu Shooting 0-1 Young Africans
 
timu zote zipo uwanjani na mpira unaweza kuanza wakati wowote kuanzia hivi sasa.
 
00' Naaam mpira umeanza kwa timu ya Ruvu Shooting kuanzisha kipute hiko.
 
Nimezisikia tambo za mzee wa simu 15 wacha tuone dkk 90' zinasemaje!
 
4' Fedhuri Maganga anapoteza nafasi ya wazi alipata kitete kutumbukiza mpira wavuni, Kevin Yondan anatokea na kuokoa mpira ule na kuwa kona.
 
10' Ruvu Shooting 0-0 Yanga
 
13' Rafael Daudi amejenga kibanda kwenye lango la Ruvu Shooting.
 
15' Gooooooooooooooooooooal
Papii Kabamba Tshishimbi anaipatia Yanga goli la kuongoza katika uwanja wa Uhuru, Dar es salaam akipokea basi mujarabu kutoka kwa Rafael Daud
Ruvu Shooting 0-1 Yanga
 
20' Ruvu Shooting 0-1 Yanga
 
21' Emmanuel Martin amepiga shuti kali nje ya box kwenda kumsalimia Klaus Kindoki na inakuwa chakula kwake na kuutuliza kwenye himaya yake.
 
24' Kadi ya njano kwa Kevin Yondani baada ya kumfanyia madhambi Shaban Msala.

refa nae binadamu, Shaibu Ninja ndiye aliyefanya foul ila kadi ikaenda kwa Yondani.
 
28' Herithier Makambo amemtengea pasi nzuri Tshishimbi anapoteza mpira ule kwa kukosa utulivu, lakini lines man anasimamisha kibendera kumaanisha ni offside.
 
30' Herithier Makambo anapiga shuti kipa anacheza mpira unamkuta Rafael Daud unagonga mwamba na mpira unatoka nje.

Ruvu Shooting 0-1 Yanga
 
Back
Top Bottom