Ligi Kuu Bara inaendelea leo katika uwanja wa Uhuru, kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Yanga. Endapo klabu ya Yanga itaondoka na pointi tatu katika mechi ya leo, moja kwa moja Yanga itaenda kuongoza ligi kwa pointi 83 wakiwa wamebakisha mechi mbili kumaliza ligi, huku ikiiacha Simba kwa pointi moja nyuma wakati huo Simba ikiwa na michezo 5 mkononi.
LINE-UPS
15' Gooooooooooooooooooooal
Papii Kabamba Tshishimbi anaipatia Yanga goli la kuongoza katika uwanja wa Uhuru, Dar es salaam akipokea basi mujarabu kutoka kwa Rafael Daud
Ruvu Shooting 0-1 Yanga
28' Herithier Makambo amemtengea pasi nzuri Tshishimbi anapoteza mpira ule kwa kukosa utulivu, lakini lines man anasimamisha kibendera kumaanisha ni offside.