Tanzania prisons kama masihara vile

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
611
Reaction score
567
Timu ya soka ya Tanzania Prisons maarufu kama Wajelajela yenye makazi yake jijini Mbeya, leo hii imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Geita Gold fc.

Mchezo huo ambao umechezwa kwenye uwanja wa Nyankumbu ulikuwa wenye ushindani mkubwa.

Kwa matokeo hayo ambayo Prisons wameyapata yamewafanya kufikisha point 31 na hivyo kuendelea kuondoka katika eneo la hatari la kushuka daraja.

Tangu timu hiyo ilipobadilisha kocha kwa kumuondoa Odhiambo na kumkabidhi Bares timu imekuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchezaji.

Mashabiki wa soka ndani ya mkoa wa Mbeya na nyanda za juu kwa ujumla wamekuwa wakiziombea timu za Mbeya city, Prisons na Ihefu sports club ziendelee kufanya vizuri kwenye michezo iliyosalia.

Tanzania Prisons wamebakisha mechi tatu ambazo ni dhidi ya Kagera sugar, KMC pamoja na Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…