SoC04 Tanzania safi bila rushwa

SoC04 Tanzania safi bila rushwa

Tanzania Tuitakayo competition threads

IBRAHIMU SALAH

New Member
Joined
Jun 14, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Ili kutokomeza rushwa na kujenga TANZANIA TUITAKAYO ni lazima tuzingatie sekta zote katika nchi yetu zinatoa huduma bora na stahiki kwa usawa pasipo rushwa kwa wananchi wote.

Zifuatazo ni njia za kupambana na rushwa katika sekta mbalimbali nchini ili kufikia TANZANIA TUITAKAYO nazo ni;
i .utoaji wa elimu ya rushwa;ili kukuza uelewa wa watanzania dhidi ya rushwa ni lazima elimu ya rushwa itolewe yaani nini maana,aina,madhara na njia za kupambana na rushwa kwa watu wote wa sekta zote maeneo yote mfano Ili kuripoti rushwa piga *113#.

ii .kukagua mifumo yetu ya teknolojia na kielektroniki kama hairuhusu mwanya wowote wa rushwa,ikihusisha mashine za ukataji risiti,reseni,tiketi mbalimbali,namba za malipo za serikali katika sekta za serikali.

iii .PCCB( taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania) ipewe nafasi katika Kila shughuri za serikali na zisizo za serikali mfano wakati wa uchaguzi Kila wakati wa kampeni PCCB ipewe warau dakika 15 za kutoa elimu ya rushwa,bungeni,mikutano ya hadhara,hafla za viongozi wa kisiasa ili kutoa elimu kuweka msisitizo kuhusu rushwa kwa wananchi.

iii .Wakati wa ukaguzi wa miradi mbalimbali ya afya,elimu,mazingira na uchumi PCCB wapewe nafasi ili kukagua chembechembe zozote za rushwa na kuripoti ili hatua stahiki zifatwe.

iv .PCCB ipewe ofisi za utendaji kazi katika ngazi za wilaya, na vijiji ili kuifikia jamii kubwa ya watu, kwasababu tuna jamii ya watu hawajui kusoma, kuandikia pia kutumia simu ivo hawawezi kupata huduma ya elimu ya rushwa kupitia vipeperushi na mitandao ya kijamii pia kutoa taarifa ya rushwa kupitia sms au kupiga simu kupitia *113#.

v .PCCB ifundishe watu na kuwatumia kwa Siri kama wapelelezi katika sekta mbalimbali nchini ili kutoa taarifa na kudhibiti rushwa kwani si kila mwananchi anao ujasiri wa kutoa taarifa kuhusiana na rushwa.

vi .Adhabu ya mtoa rushwa na mpokea rushwa itangazwe hadharani ili kuweka msisitizo kwa wengine kuogopa rushwa lakini pia Mali zao zitaifishwe na serikali.

vii .kuanzisha na kuziwezesha kifedha asasi zingine za serikali na zisizo za serikali ili kushirikiana na PCCB katika utendaji kazi.mfano anti corruption voices iliyotimiza miaka miwili tangu kuanzishwa kwake ikiwa na kauli mbiu "badili tabia sepesha rushwa".

viii .PCCB iwe na watendaji kazi wake katika Kila wizara za serikali ya Tanzania ili kupambana na rushwa.
"TANZANIA BILA RUSHWA. INAWEZEKANA, TANZANIA TUITAKAYO TUTAIFIKIA"
 
Upvote 1
Back
Top Bottom