Tanzania sasa tuwe na siku tatu za kupumzika katika wiki moja

Kakende

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2012
Posts
2,741
Reaction score
1,232
Tangu mchakato wa kutoa maoni ya KATIBA uanze, baadhi ya watanzania kwa kupitia Radio fulani pia makongamano mbalimbali ya katiba wanapenda sasa nchi iwe na siku tatu za kupumzika hili pia waislam nao wapate nafasi ya ibada ili iwe haki sawa. Siku ya Ijumaa (Waislam), Jumamosi (Wasabato), Jumapili( Madhehebu mengine ya Kikristu)

Nchi kama Saudi arabia mapumziko yao ni Alhamis na Ijumaa, Nchi za Ulaya Mapumziko yao ni Jumamosi na Jumapili. Hapa kwetu ni Jumamosi na Jumapili. Sina uhakika kama Jumapili na Jumamosi zipo kwenye Katiba ya sasa au ni mfumo tulio urithi kwa wakoloni.

Mimi binafsi naona kama siku ya mapumziko itaanzia Ijumaa basi tutakuwa tumeweka rekodi ya dunia kwa kurest. We unasemaje?
 
hakuna shida taasisi za kikristo kama shule, benki zitaendelea kama kawa kwenye interview ukisema huwez fanya kazi ijumaa basi imekula kwako
 
Cdhani kama itawezekana! Kwani nchi kama saudia,ni nchi za kidini,Tanzania cio nchi ya kidini
 
Ili kuondoa hii mitafaruku basi ninapendekeze siku neutral. Mimi napendekeza tupumzike siku za Jamanne na Jumatano ili kuondoa mang'uniko. Disadvantege yake ni kwamba nchi partners tutakuwa tunapishana nao mapumziko hivyo mara nyingine shughuli za kiofisi na nchi wahisani/partners zitakwama siku za mapumziko kama itakuwa Jumanne na Jumatano.
 
Kafanye utafiti vizuri, hakuna nchi duniani zinazoshabihiana katika siku za kitaifa. Kila nchi ina siku yake kitaifa na hatujasikia wakikosa fursa za kushirikiana kwa hilo. Vivyo hivyo nchi zote za kiarabu ambazo ndio mdau mkuu wa maendeleo hapa duniani hasa unapoakisi suala la nishati basi wao wana mapumziko yao ambayo hayalingani na nchi za kikristo. Mfano sikukuu za Eid zote, Dubai ni zaidi ya siku nne, Oman wiki moja, Saudia zaidi ya siku nne n.k.

Unajua mmejenga stereotype kwa waislamu na mkawadharu kwa kila hoja waletayo. Kumbukeni hawa ni wananchi wa Tanzania, lakini vilevile wanayohaki ya kuthaminiwa na kupata stahiki za kiraia. Kuishi kwetu kwa amani kunatokana na wananchi hawa mnaowadharau kuvumilia tu. Tazama kwa mantiki tu ya kawaida, iwapo Wasabato wanapata Jumamosi kwenda kuabudu kwa nafasi, madhehebi mengine ya kikristo wanapata siku ya Jumapili kwenda kuabudu, iweje leo waislam waombe Ijumaa kutambuliwa rasmi iwe kioja? Kumbuka kama unatakiwa upate haki wewe, na mwingine naye umpe. Sote ni wananchi.
 
Tangu mchakato wa kutoa maoni ya KATIBA uanze, baadhi ya watanzania kwa kupitia Radio fulani pia makongamano mbalimbali ya katiba wanapenda sasa nchi iwe na siku tatu za kupumzika hili pia waislam nao wapate nafasi ya ibada ili iwe haki sawa. Siku ya Ijumaa (Waislam), Jumamosi (Wasabato), Jumapili( Madhehebu mengine ya Kikristu)

Nchi kama Saudi arabia mapumziko yao ni Alhamis na Ijumaa, Nchi za Ulaya Mapumziko yao ni Jumamosi na Jumapili. Hapa kwetu ni Jumamosi na Jumapili. Sina uhakika kama Jumapili na Jumamosi zipo kwenye Katiba ya sasa au ni mfumo tulio urithi kwa wakoloni.

Mimi binafsi naona kama siku ya mapumziko itaanzia Ijumaa basi tutakuwa tumeweka rekodi ya dunia kwa kurest. We unasemaje?

kupumzika nikuamua kama umetosheka pumzika siku zote kabisa,watanzania tunapenda sana kupumzika hata wakenya wanatushinda,ukimuajiri mtanzania ujiandae kwa uzuru kila siku,nenda nchi za wazungu uone kama wanazingatia siku za mapumziko au vp?tutengeneze wasomi wakutosha ili kuwe na some off days katika kazi but kwa upande wangu hata hiyo j-mos na j-pil mi ninge cancel kabisa
 
Kazi ipo.........

:A S angry:Haki haipatikani kwa mabadiliko ya katiba au kubeba mabango, bali hupatikana kwa kuuondoa mfumo kwa mikono yetu na nguvu zetu:glasses-nerdy:
 
Kafanye utafiti vizuri, hakuna nchi duniani zinazoshabihiana katika siku za kitaifa. Kila nchi ina siku yake kitaifa na hatujasikia wakikosa fursa za kushirikiana kwa hilo. Vivyo hivyo nchi zote za kiarabu ambazo ndio mdau mkuu wa maendeleo hapa duniani hasa unapoakisi suala la nishati basi wao wana mapumziko yao ambayo hayalingani na nchi za kikristo. Mfano sikukuu za Eid zote, Dubai ni zaidi ya siku nne, Oman wiki moja, Saudia zaidi ya siku nne n.k.

Unajua mmejenga stereotype kwa waislamu na mkawadharu kwa kila hoja waletayo. Kumbukeni hawa ni wananchi wa Tanzania, lakini vilevile wanayohaki ya kuthaminiwa na kupata stahiki za kiraia. Kuishi kwetu kwa amani kunatokana na wananchi hawa mnaowadharau kuvumilia tu. Tazama kwa mantiki tu ya kawaida, iwapo Wasabato wanapata Jumamosi kwenda kuabudu kwa nafasi, madhehebi mengine ya kikristo wanapata siku ya Jumapili kwenda kuabudu, iweje leo waislam waombe Ijumaa kutambuliwa rasmi iwe kioja? Kumbuka kama unatakiwa upate haki wewe, na mwingine naye umpe. Sote ni wananchi.

Peculiar,peculiar!
Kwanza Jmosi ni nusu siku ya kazi kikatiba, the fact is, kwa jinsi dunia inavyozidi kuwa kijiji kwenye cloud, ndivyo akili zinatakiwa ziifuate katika kufikiria, ukijiwezesha kupumzika hata wiki nzima its fare for you! Lakini, inapokuja kufikiria kwa undani, uwaekezaji, maingiliano ya kibiashara yaani e-world n.k. utaona ku-rest siku tatu kwa wiki is THE most peculiar idea of the history of a young country. Fikiria una cheque bank inayotakiwa kuiva say siku saba za kazi, fikiria tena una tangazo muhimu la kiserikali unatakiwa kulitangaza siku saba za kazi, fikiria Mahakama kuu inatakiwa kuendesha kesi zake siku za kazi tu, how can you be such complacent, ukitaka kupumzika its a cool idea ukapumzika kivyako, we are i n the mostly competatively growing nation, do't take things lightly. Msituvute mashati, nyiye restini tu.
 
Tangu mchakato wa kutoa maoni ya KATIBA uanze, baadhi ya watanzania kwa kupitia Radio fulani pia makongamano mbalimbali ya katiba wanapenda sasa nchi iwe na siku tatu za kupumzika hili pia waislam nao wapate nafasi ya ibada ili iwe haki sawa. Siku ya Ijumaa (Waislam), Jumamosi (Wasabato), Jumapili( Madhehebu mengine ya Kikristu)

Nchi kama Saudi arabia mapumziko yao ni Alhamis na Ijumaa, Nchi za Ulaya Mapumziko yao ni Jumamosi na Jumapili. Hapa kwetu ni Jumamosi na Jumapili. Sina uhakika kama Jumapili na Jumamosi zipo kwenye Katiba ya sasa au ni mfumo tulio urithi kwa wakoloni.

Mimi binafsi naona kama siku ya mapumziko itaanzia Ijumaa basi tutakuwa tumeweka rekodi ya dunia kwa kurest. We unasemaje?

Na sisi waumini wa Bahai tunaomba Tuesday iwe siku ya mapumziko kwani ndio siku yetu takatifu
 
Yaani watu wanataka kuongeza masaa na siku za kufanya kazi nyie mnaongelea kupunguza siku za kufanya kazi?!

Kweli nimeamini .... What an African likes best is to do nothing for six days and to rest on seventh
 
Wapagani na waabudu mizimu sie tutapumzika lini????
Vipi marasta fari???
Vipi YEHOVA witness??
 
Kafanye utafiti vizuri, hakuna nchi duniani zinazoshabihiana katika siku za kitaifa. Kila nchi ina siku yake kitaifa na hatujasikia wakikosa fursa za kushirikiana kwa hilo. Vivyo hivyo nchi zote za kiarabu ambazo ndio mdau mkuu wa maendeleo hapa duniani hasa unapoakisi suala la nishati basi wao wana mapumziko yao ambayo hayalingani na nchi za kikristo. Mfano sikukuu za Eid zote, Dubai ni zaidi ya siku nne, Oman wiki moja, Saudia zaidi ya siku nne n.k.

Unajua mmejenga stereotype kwa waislamu na mkawadharu kwa kila hoja waletayo. Kumbukeni hawa ni wananchi wa Tanzania, lakini vilevile wanayohaki ya kuthaminiwa na kupata stahiki za kiraia. Kuishi kwetu kwa amani kunatokana na wananchi hawa mnaowadharau kuvumilia tu. Tazama kwa mantiki tu ya kawaida, iwapo Wasabato wanapata Jumamosi kwenda kuabudu kwa nafasi, madhehebi mengine ya kikristo wanapata siku ya Jumapili kwenda kuabudu, iweje leo waislam waombe Ijumaa kutambuliwa rasmi iwe kioja? Kumbuka kama unatakiwa upate haki wewe, na mwingine naye umpe. Sote ni wananchi.
Lakini mkuu QURAN inawakataza wao kupumzika siku ya ibada...inawaamuru waislmu woote mara ya swala watawanyike fasta wakajitafutie riziki...hili unalichukuliajee...
 
Kafanye utafiti vizuri, hakuna nchi duniani zinazoshabihiana katika siku za kitaifa. Kila nchi ina siku yake kitaifa na hatujasikia wakikosa fursa za kushirikiana kwa hilo. Vivyo hivyo nchi zote za kiarabu ambazo ndio mdau mkuu wa maendeleo hapa duniani hasa unapoakisi suala la nishati basi wao wana mapumziko yao ambayo hayalingani na nchi za kikristo. Mfano sikukuu za Eid zote, Dubai ni zaidi ya siku nne, Oman wiki moja, Saudia zaidi ya siku nne n.k.

Unajua mmejenga stereotype kwa waislamu na mkawadharu kwa kila hoja waletayo. Kumbukeni hawa ni wananchi wa Tanzania, lakini vilevile wanayohaki ya kuthaminiwa na kupata stahiki za kiraia. Kuishi kwetu kwa amani kunatokana na wananchi hawa mnaowadharau kuvumilia tu. Tazama kwa mantiki tu ya kawaida, iwapo Wasabato wanapata Jumamosi kwenda kuabudu kwa nafasi, madhehebi mengine ya kikristo wanapata siku ya Jumapili kwenda kuabudu, iweje leo waislam waombe Ijumaa kutambuliwa rasmi iwe kioja? Kumbuka kama unatakiwa upate haki wewe, na mwingine naye umpe. Sote ni wananchi.

Yaani hata upuuzi wa namna hii unauita HOJA?

Wapi kwenye dini yako kumeandikwa kwamba upumzike Ijumaa? Shida yenu sio kupumzika, bali shida yenu ni kwa nini Wakristo wanasali Jumapili.

Ukiwa na akili timamu huwezi kushabikia nchi ikae mguu juu siku 3 kwa wiki na ukasema unataka kuendelea. Unalalamika kuwa unadharauliwa lkn hapo hapo haya ndio mawazo yako, ambayo si mema kwa maendeleo ya nchi.

Jumapili si siku ya Wakristo kusali. Wakristo wanasali siku zote, ila kwa kuwa Jumapili ni Public Holiday, basi ikaonekana itumike kufanya Dominika. Sasa sijui kwa nini wewe mwenye dini ya kusali siku moja usiitumie hiyo Jumapili kusali badala ya kunung'unika kama toto la mtaani.
 
Back
Top Bottom