Tanzania yangu niipendayo ni nchi iliyobarikiwa rasilimali nyingi kiasi Cha kuwa na uwezo wa kufika uchumi wa juu ndani ya miaka 20 ijayo.
Nikianza na mabadiliko yanayopaswa kufanyika kwenye sekta ya kilimo kwa kua kilimo ni uti wa uzalishaji Mali kwenye nchi yetu kinapaswa kufanyika kisasa zaidi bajeti ya wizara ya kilimo inapaswa kuwa kubwa zaidi ya iliyopo Sasa.
Bajeti ya kilimo inapaswa kuhakikisha zianpatikana mashine zinazorahisisha kilimo Hadi katika vijiji kabisa kwa wakulima wadogowadogo na kuwezesha kutumika kwake mashine kama trekta na mashine za kuvunia mazao zikipelekwa mpaka kwa mkulima wa ekari Moja kutaboresha kiwango cha mazao anachovuna mwaka mpaka mwaka na kuinua hali yake ya kiuchumi Hali ilivo mpaka Sasa si rafiki kabisa kwa mkulima wa Tanzania kwa maana wanaopewa kipaumbele ni hao wakulima wakubwa wenye maeneo makubwa na hivyo kuboresha Hali zao za kiuchumi na kuzidi kuwanyonya wakulima wadogowadogo.
Ruzuku ya mbolea inapaswa kutolewa na Serikali kwa wakulima wote bila kujali ni wakulima wa Mazao ya biashara Wala mazao ya chakula kwa maana mazao yote yanaleta faida kubwa sana katika nchi wakati wa kuuzwa.
Uzalishwaji wa wataalam wa kilimo uongezwe na ajira zao zitolewe kwa wingi Kuna uwezekano mkubwa kabisa kua nchini Tanzania wataalam wa masuala ya kilimo ni wengi sana lakini hawapewi ajira kwa ajili ya kutumia juzi walizozipata mashuleni kwao hivyo kupelekea kujishughulisha na shughuli zinginezo kabisa tofauti na kilimo vijiji vingi nchini Tanzania vinakosa wataalam wa masuala ya kilimo suala linalopelekea kilimo kufanyika katika ubora wa chini na kusababisha mavuno ya chini na kuzidi kunyongonyesha uchumi wa wakulima wadogo wadogo
Masoko, nchini Tanzania masoko ya mazao ya kilimo yamekua ya kukatisha tamaa kwa mkulima mdogo mdogo kwa mfano kwa mwaka huu zao la mpunga lilishoka Bei mkoani geita mpaka tsh 36000 kwa kipimo Cha dumu la lita 20 suala ambalo linatia hasara kubwa kwa wakulima ushauri wangu kama serikali itakua na uwezo wa kununua mazao ya wananchi wakati wa mwanzo kabisa wa mavuno Kila eneo na kuacha misingi ya Bei elekezi maeneo hayo itapunguza Hali mbovu ya uchumi katika maeneo yote nchini.
Suala lingine linalohitaji kubadilika katika Tanzania yangu ni namna ya kukusanya Kodi. Mfumo uliopo wa ukusanyaji Kodi nchini wa kielektroniki ni mzuri sana lakini unaweza kua unapata changamoto kukusanya kiwango sahihi cha Kodi kwa kua kuna biashara ambazo hazitoi risiti automatically ushauri wangu kwa nchi Ili ipate kiwango sahihi cha kodi inapaswa kutunga sheria inayolazimu Kila mwananchi kuwa na kadi ya malipo yaani mfanyabiashara yeyote amiliki kifaa cha kielektroniki kinachosoma kadi ya malipo hata kama serikali itatengeneza na kuuza vifaa hivyo kwa Bei ndogo lakini vitainua Kodi kwenye nchi yetu pesa taslimu isitumike kulipia bidhaa yoyote sokoni, hili suala likifanyika nchini kwetu ndani ya mda mfupi nchi itakusanya Kodi halali na itafanyia shughuli za kimaendeleo Kodi hiyo na nchi itahamia kwenye uchumi wa juu ndani ya mda mfupi
MFUMO HUU UFANYIKE VIPI?
Kwanza Kila mfanyabiashara asajili biashara yake kwenye serikali kuanzia biashara ndogo ndogo mpaka kubwa kuepusha mashine hizi kuuzwa kwa Bei kubwa na pia ofisi za serikali kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka ngaz ya mkoa ziruhusiwe kufanya usajili huo Ili kupunguza msururu wa watu mashine zitengenezwe kulingana na viwango vya mtaji vya wafanyabiashara serikali itengeneze kadi zisizofungamana na benki yoyote ile na mtandao wowote ule nikiwa na maana pesa inaweza kuwekwa na mtandao wowote na benki yoyote bila makato au makato nafuu hiyo kadi iruhusiwe kumilikiwa na mtu wa rika yoyote nchini cheti Cha kuzaliwa kinaweza tumika kutengeneza kadi hiyo Ili Kila mtu anaponunua au kuuza kadi itumike kufanyia malipo hili litaongeza ukusanyaji wa Kodi kwenye nchi yetu na shughuli nyingi za mAendeleo zitafanyika na nchi itaendelea.
Mabadiliko katika mfumo wa uongozi nchi yetu imefanikiwa kupata viongozi katika awamu sita tofauti za Marais Kila kiongozi huja na sera zake na misimamo yake na hufanya kazi lakini nchi yetu haijafika katika kiwango tunachokihitaji maoni yangu nchi yetu Inahitaji mabadiliko yafuatayo katika suala la uongozi Moja kabisa ni kipimo cha ufanisi wa kiongozi wa juu wa Serikali yaani rais sheria inapaswa kuwekwa itakayohitaji chama chochote cha kisiasa kinachotoa raisi kuweka kipimo cha uchumi mfano kutoa nchi katika bajeti ya mwaka ya trilioni 20 mpaka bajeti ya trilioni 35 ndani ya miaka mitano endapo raisi atashindwa kufikia malengo yaliyowekwa asirudi madarakani kwa miaka mingine mitano chama kinapaswa kuteua kiongozi mwingine wa kuenda madarakani na kipimo halisi kiwekwe pia sheria ya kuweka ukomo wa uwakilishi katika mabunge yote yaJamhuri ni suala la mhimu sana Ili kuruhusu mabadiliko ya uongozi katika majimbo.
Jambo lingine mhimu ni kufungwa kwa camera za usalama barabarani Ili kuzuia vitendo vya kiuhalifu ikiwemo rushwa na ajali barabarani.
Yakifanyika hayo TANZANIA ya uchumi wa juu inaezekana ndani ya miaka 20 mpaka 25.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.AMEN

Upvote
2