Tanzania - Somalia zasaini hati nne za makubaliano ya ushirikiano

Tanzania - Somalia zasaini hati nne za makubaliano ya ushirikiano

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
TANZANIA - SOMALI ZA ZASAINI HATI NNE ZA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

Waziri Kombo apongeza mageuzi ya uchumi na utulivu wa kisiasa unaoendelea nchini humo

Wautaja umoja amani na usalama wa Tanzania kuwa ni mfano wa kuigwa Afrika

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Shirikisho la Somalia zimesaini hati nne za makubaliano ya ushirikiano katika mkutano uliofanyika jijini Mogadishu leo tarehe 19 Disemba, 2024 chini ya uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Balozi Ahmed Moalim Fiqi.

mini_magick20241219-40130-cne5hc.jpg


Hati hizo nne zilizosainiwa zimehusisha Ushirikiano wa jumla, sekta ya Utalii, Ulinzi na Afya. Hatua hiyo inalenga kukuza ushirikiano wa kidiplomasia na uchumi sambamba na kuboresha utoaji huduma kwenye sekta hizo kwa manufaa ya raia wa mataifa yote mawili.

Waziri Kombo akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini wa hati hizo Waziri Kombo ameeleza Tanzania imepiga hatua kubwa katika utoaji wa huduma za afya ambapo kupitia makubaliano hayo Somalia watapata fursa ya kunufaika na huduma mbalimbali zinazopatikana nchini kwenye sekta hiyo ikiwemo matibabu, kununua madawa na vifaa tiba na mafunzo.

mini_magick20241219-40130-4odrum.jpg


Aliendelea kueleza kuwa Serikali za pande zote mbili zinatambua kuwa ili wananchi waweze kunufaika na fursa hizo ni muhimu kuhakikisha huduma za mawasiliano na usafiri kati ya Tanzania na Somalia zinaimarishwa. Hivyo amehimiza kuharakishwa kwa mazungumzo yanayoendelea ili huduma ya usafiri wa moja kwa moja kwa njia ya anga kati ya Dar es Salaam na Mogadishu ianze kupatikana mapema iwezekanavyo.

Aidha Waziri Kombo ameelekeza watendaji kuandaa utaratibu maalumu wa kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa mikataba mamkubaliano yaliyofikiwa huku akihimiza kuwa nataka kuona ikitekelezwa kwa vitendo.

mini_magick20241219-40130-o1jbds.jpg


Ushirikiano huu utasaidia mataifa yetu kufikia malengo yake ya kiuchumi sambamba na kukidhi matarajio ya Wakuu wa Nchi zetu ambao dhamira yao nikuona ustawi wa uchumi wa wananchi kupitia fursa zainazotokana ushirikiano huu. Hivyo ni muhimu kwetu sote kuhakikisha makubaliano haya yanatekelezwa kwa vitendo. Alieleza Waziri Kombo.
 

Attachments

  • mini_magick20241219-40130-xc3diz.jpg
    mini_magick20241219-40130-xc3diz.jpg
    68.7 KB · Views: 3
  • mini_magick20241219-40130-eorula.jpg
    mini_magick20241219-40130-eorula.jpg
    58.8 KB · Views: 3
  • mini_magick20241219-40130-5ybfc7.jpg
    mini_magick20241219-40130-5ybfc7.jpg
    70.7 KB · Views: 3
  • mini_magick20241219-40130-bzm9gb.jpg
    mini_magick20241219-40130-bzm9gb.jpg
    81.5 KB · Views: 2
  • mini_magick20241219-40130-tc9obw.jpg
    mini_magick20241219-40130-tc9obw.jpg
    72.4 KB · Views: 2
  • mini_magick20241219-40130-ufonfg.jpg
    mini_magick20241219-40130-ufonfg.jpg
    74.2 KB · Views: 2
  • mini_magick20241219-40130-ttk2mh.jpg
    mini_magick20241219-40130-ttk2mh.jpg
    75 KB · Views: 2
Kwani nyie watu mmekuwaje siku hizi!? "Somali" ndio kitu gani hiko!?
 
Back
Top Bottom