Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Tanzania ni nchi ya 14 duniani kwa uzalishaji wa gesi asilia ikizalisha 0.05% ya gesi yote inayozalishwa duniani. Uzalishaji wa gesi nchini umeongezeka kwa asilimia 9 mwaka 2023 kulinganisha na mwaka 2022. Mataifa yanayoongoza kwa uzalishaji wa gesi asilia ni Marekani, Urusi na Iran.
Kampuni kubwa inayochimba gesi nyingi zaidi nchini ni Orca Energy ikifuatiwa na Maurel & Prom na nafasi ya tatu ikifungwa na Wentworth Resources. Mkoa wa Mtwara unaongoza kuwa na visima vingi vya gesi nchini.
Visima vikubwa nchini ni Songosongo na Mnazi Bay vilivyoanza uzalishaji mwaka 2004 na 2006 mtawalia. Visima vikubwa ambavyo vipo katika hatua ya uendelezaji na vinatarajia kuanza uzalishaji mwaka 2029 ni Zafarani Complex(Exxon Mobil; Equinor), Block 1(PT Medco Daya Abadi Lestari; Shell; Pavilion Energy), Block 4(PT Medco Daya Abadi Lestari; Shell; Pavilion Energy) na Ntorya(ARA Petroleum; Aminex) kitachoanza 2025
Tanzania inatarajia kuanza kuuza kiwango kikubwa cha gesi nje ya nchi baada ya kuingia mkataba na Equinor(Norway) na Shell(Uingereza) ambapo itawezesha ujenzi wa mradi wa LPG wenye thamani wa dola za kimarekani bilioni 30 unaotarajiwa kuanza kazi 2029-2030.
Ujenzi wa mradi wa kiwanda cha LPG ulicheleweshwa na Rais John Magufuli huku mkurugenzi wa Equinor Tanzania akisema walikumbana na vikwazo lakini walisuluhisha na Serikali na anatarajia gesi itatoa fursa kubwa.
Pia, Soma=> Rais Magufuli: Mabepari wametunyang'anya gesi yetu hatuwezi kuitumia kwa uhuru