Tanzania taifa la mapenzi,watu wanawaza mapenzi mda wote.

Mapenzi ndio kila kitu, Watu wanafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya mapenzi, watu wanasoma kwa bidii mapenzi watu wanajenga nyumba nzuri kwa kutaka mapenzi, watu wananunua magari mazuri yoote hayo mapenzi tu wengine wanakuwa fisadi mapenzi.
 
Nawe MR. sitaki mapenzi kimekuleta nini huku ?
 
Dogo ushaambiwa pesa,pombe, siasa na wanawake ndio inayofanya watu tunawehuka sasa nini tena zaidi

Wewe kama ni NERD peke yako dogo
 

Mkuu Inzi umeninukuu vibaya kwani hakuna sehemu nimeandika tuache jukwaa hili na twende jukwaa la siasa,sijasema popote kuhusu kuamia jukwaa fulani ila nimesema majukwaa mengine hata kwa kupotea hautamwona mtu ila tu kwenye hili la mapenzi

La sports hamna,la malalamiko hamna,la elimu hamna,la habari hamna,la siasa hamna,la daktari hamna,yaani wewe masaa 24,siku 7 wiki 4 zote ni wewe na mapenzi mapenzi na wewe...are you addicted?wewe utakuwa unaishi sayari gani iliyozungukwa na mapenzi tu?kwamba kweli kichwa chako kina ukilema wa mapenzi?kama ndivyo basi kuna kitu hakiko sawa.
 
Ya mwambie ukweli Matola !!
mambo mengine ni kutojua tu ,jukwaa linaitwa MMU, Na sio ngono ka anavyofikiria afu mwambie izo kauli tarabu
cause si wengine tuko kwenye ndoa zetu isitoshe tunapata matilio za nguvu hapa MMU!!!
 

mapenzi yanachukua assilimia kubwa ya maisha ya mwanadamu yeyote,hakuna mtu asiyehitaji kupendwa,
familia-ni upendo
jamii-ni upendo
nchi-ni upendo
dunia ni upendo
na hata maisha ni upendo
kwa maana hiyo hatuwezi kuacha kuwaza mapenzi na ngono hiyo mimi nakataa,tena wewe ndo unawaza ngono mpaka unachanganyikiwa ndo maana umeanzisha mada hii
 
Mi nadhani mtoa mada anajiuliza sababu ya jukwaa hili kujaa watu wengi,ila kuna ka ukweli kwenye mada yake,tuwe wakweli!
 
Mii nadhani ndio maana nchi ina amani (kama kweli ipo lakini) ...maana mtu akitaka kuanzisha choko choko akikumbuka tu kwenye vita mapenzi hayana nafasi basi anaahirisha mwenywewe
 
siasa mi nadhani ni interest ya mtu..
Mpira ama michezo kwa ujumla,ni interest pia..
Habari za biashara uchumi,sheria,lugha,etc.. kadhalika...

Lakini mapenzi yanawagusa wote ........ Labda nijisahihishe kwa kusema wengi...
 

Na kwa nini walibadili jina la jukwaa kuliita la ngono? Kwanini?
Wala hatuongeagi masuala ya ngono,mfano kuna wanaume wana maumbile marefu au wanawake wana maumbile yasiyoridhisha kwa hali fulani.... Hakuna...

Kuna watu wana matatizo,sio kichwani peke yake,bali athari za matatizo binafsi ya kifamilia..
 

Utawaweza basi. . .watu wengine hua wanaongea alimradi nao waonekane wameongea. Ukifuatilia sana utaona hata yale maswali ya msingi hawajibu, wanabaki kun'ang'ania kitu kile kile kisicho na kichwa wala miguu.
 
Mungu alikuwa anakusanya kusanya vifaa vyake tayari kwa kufunga kazi ya uumbaji,kugeuka nyuma kumuona Adam amejikunyata kama mtu aliyeshikwa na na ngiri,hivyo roho ya huruma ikamjia,akarudi akamchomoa ubavu wa kushoto hapo akamletea msaidizi wake Eva,unahisi alimleta amsaidie nini?Mapenzi yana run dunia baaab!!!!
 
Bora useme wewe mkuu maana nikisema mimi nitaonekana mnafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…