KILIMO ni mchakato wa kulima mazao ya chakula na mazao biashara pamoja na kufuga wanyama.Hapo mwanzo ilifahamika tu kwamba kilimo kinahusisha ulimaji wa mazao pekee lakini kutokana na mabadiliko na maendeleo ambayo yamejitokeza hivi sasa, kilimo kinajumuisha Ulimaji wa mazao na Ufugaji wa mifugo.
Katika Nchi ya Tanzania takribani asilimia themanini na tano (85%) ya watu wanajishughulisha na Kilimo. Hili lipo wazi kabisa kuwa, kwa wakazi wengi kilimo ni Uti wa mgongo na watu wengi mnoo wamejiajiri kwenye sekta hii adhimu.
Utekelezaji wa aina ya kilimo ufanyikao, umegawanyika katika sehemu kuu mbili.Moja, kilimo kidogo ambacho huanzia hekali moja mpaka kumi lakini pia kuna kilimo kikubwa ambacho hichi huanzia hekali mia moja na kuendelea.
Nizungumzie hasa kilimo cha ulimaji wa maeneo madogo ambacho ndicho idadi kubwa ya watu wanashiriki kufanya hasa, maeneo ya vijijini au maeneo yaliyopo mbali na mjini, kwanza huweza kulima zaidi mazao ya chakula kama vile mtama,Uwele na mahindi.
Hapa nitakugusia miongoni mwa Wilaya inayopatikana mkoa wa Dodoma iitwayo Mpwapwa ambapo wakazi wengi katika wilaya hiyo wanajishughulisha na kilimo cha mtama na Uwele haya ndiyo mazao yao pendwa kwa ajili ya kuweza kujipatia mahitaji muhimu kama vile chakula.
Wahenga walinena "Siku zote jembe halimtupi mkulima" hakika huu usemi unaishi mpaka hivi sasa katika kizazi hichi.Mazao huvunwa vizuri kutokana na mazao hayo kustahimili hali mbalimbali ambayo hutokea kama upungufu wa mvua ambao hutokea mara kwa mara.
CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA WAKULIMA WADOGO NCHINI TANZANIA.
Ikiwemo Wilaya Mpwapwa inayopatikana Mkoa wa DODOMA.
Mosi, ukosefu wa fedha za kutosha: hii ni miongoni mwa changamoto inayokuwakuta wakulima wadogo wadogo ambapo hukosa pesa ya kununua nyenzo mbalimbali kwa ajilu ya kilimo mfano mbolea,madawa na hata kukodisha eneo kubwa ambalo litamuwezesha mkulima kupata mazao mengi zaidi.Lakini kutokana na ukosefu wa pesa husababisha kupata mavuno madogo.
Pili, Uwepo wa miundombinu isiyorafiki: watu wengi wanaojishughulisha na kilimo wanaishi mbali na mjini hivyo miundombini kama vile barabara bado ipo chini sana na huwa ni tatizo kubwa hasa kipindi cha mvua ambapo husababisha kukosekana kwa huduma muhimu.Licha ya hivyo miundombinu ndiyo chachu ya maendeleo sehemu yeyote ile kwani huhusika zaidi katika kusafirisha malighafi kutoka shamba kwenda sokoni.
Tatu, uwepo wa matumizi hasi wa sayansi na teknolojia: Mfano wakulima wengi wadogo wadogo bado wanatumia jembe la mkono ambapo kwao wao inakua ni ngumu sana kufikia mafanikio ukilinganisha na wale wanaotumia trekta na nyenzo nyingine muhimu katika kilimo.
SULUHISHO LA KUONDOKANA NA CHANGAMOTO HIZO:
Kwanza, wakulima wadogo wadogo wote lazima waunde vikundi au kikundi ili kuwawezesha kupata mikopo nafuu na yenye riba ndogo au isiyo na riba kwa malengo na madhumuni thaabiti ya kukuza na kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo.
Pili,uboreshaji na ujengaji wa miundombinu kama vile barabara ili kuweza kufanikisha shughuli zote za usafirishaji wa malighafi na bidhaa pasi na kuwapo kwa changamoto yeyote
Tatu, Lakini pia serikali kuwaunga na kuwashika mkono wakulima wadogo wadogo kwa kuwapunguzia kodi , pia kuwapa mikopo na misaada mingine ya muhimu utayowawezesha kuongeza uzalishaji zaidi.
Nne, Vile vile ni vema wakulima wadogo wadogo wapewe elimu stahiki kuhusu maswala ya kilimo ili waweze kufanya uzalishaji wenye tija na kupata faida yenye kukidhi haja ya mahitaji.
Hitimisho: ikiwa kama sekta ya kilimo itapewa kipaombele kwa kiasi kikubwa Mkoa wa Dodoma na Tanzania kiujumla itasaidia kutokea kwa mambo yafuatayo kama vile ongezeko kubwa la ajira kwa vijana na kila aina ya rika, ukuaji wa viwanda kutokana na upatikanaji wa malighafi, kukua na kupanuka kwa biashara ndani na nje ya nchi.

Upvote
2