Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kyakya waniacha hoi,
Na hilo wazo lako,
Nimejaribu kuwaza,
Hasira zikanipanda,
Wageni uliowataja,
Wamekaribishwa na mjombako,
Ndugu yake na mamayo!
Mikataba kawapelekea,
Kawafuata ughaibuni,
Kwenye hoteli za fasheni.
Kosa lao nini?
Hebu nijuze leo.
Na hao wenyeji wawasema,
Kwa kura zako umewachagua,
Tisheti ulivalishwa,
Na buku-jero ukasunda,
Sasa leo waliani,
Wanapokuteketeza,
Acha warudishe mtaji,
Na faida wajazie,
Usilie bwana Kyakya,
Wavuna ulichopanda.