Tanzania Tehama inaimbwa lakini vigogo wanaikataa kwasababu inawanyima ulaji?

Tanzania Tehama inaimbwa lakini vigogo wanaikataa kwasababu inawanyima ulaji?

MtotoKautaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2018
Posts
373
Reaction score
895
Enzi za Anko Magu TRC walikuwa na online system ya kukata tickets, ile system ilikuwa rahisi sana, simple yani unaenda station kupanda train tu.

Ukienda kukatia ticket station basi umependa mwenyewe. Mimi mwaka 2017 mpka 2021 nilikuwa muumini sana wa safari za train kama nakuwa sina haraka kwasababu ni usafiri ninaouappreciate sana.

It was just like 5-10 mins ticket yako unaenda kuiprint au unaweza kuwa nayo kama soft copy kwenye cm na safari inakuwa poa tu.

Sasa kwanzia pale mwenda zake alipotuaga na mfumo ni kama alienda nao mpka leo unaambiwa "this service is not available" 😄😄😄

Kuna madili wanapigaga unakuta ticket wanakuwa nazo pale station halafu either wanapewa watu maalumu kwa upendeleo au rushwa. Ukichelewa kidogo kupanga folen bas jua ticket utaipata kwa kulipa pesa kubwa tofauti na kawaida au utaikosa kabisa. Ukizingatia train kwa asilimia kubwa ni usafiri wa watu wa hali ya chini japo siyo wote.

Viongozi wa tanzania kuweni na mioyo laini tokeni kwenye enzi za kujilimbikizia mipesa wenyewe na familia zenu. Spread smile to your people mbona maisha ni simple tu.

Tunaishi mara moja jamani kama una nafasi ya kumpa tabasamu mtu fanya hivo na maisha yako yatakuwa yenye furaha na baraka tele sasa katika kila kitu wewe unawaza kupiga tu nakujilimbikizia wewe na familia yako huo ni ushamba.
 
Mtz anachojuwa ni kukata uno
Huku akicheza komasaza

Ova
 
Back
Top Bottom