Tanzania tele-high school

SolarPower

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
223
Reaction score
27
Napendekeza kama Taifa tuanzishe shule maalum ya Kidato cha Tano na Sita ambayo itakuwa inatoa mafunzo yake kwa taifa zima kwa saa 24 kila siku kupitia njia ya Televisheni na Redio kwa kushirikiana na TBC na vituo vingine vya Redio na Televisheni hapa nchini. Kwa upande wa TBC pekee, zianzishwe CHANNELS za Elimu zisizopungua tatu katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Shule hii inapendekezwa imilikiwe kwa pamoja kati ya TAMISEMI, WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI NA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA.

Masomo yanayopendekezwa kufundishwa na shule hii maalum ni PHYSICS; CHEMISTRY; BIOLOGY; MATHEMATICS; ECONOMICS; GEOGRAPHY AND HISTORY. Kutoka katika masomo haya SABA tunaweza kuwa na combinations zaidi ya 20 kama vile PBM; PHM; EPM; EBM; BGM; ECM n.k.

Pia inapendekezwa kuwe na vipindi maalum kila siku vya kutufundisha ipasavyo sisi Watanzania Lugha ya Kingereza ili tuweze kuiongea na kuiandika kwa ufasaha.

Nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…