Nchii hii ni tajiri sana kwa kila kitu lkn hakuna anayejali si sisi raia tunaoshabikia na kupiga umbea kila kukicha kuhusu mafisadi bila kuchukua hatua zozote, wala hawa viongozi wetu wanaojali matumbo yao na jamii zao.
Mao mwenyekiti wa uchina alilazimisha watu wafanye kazi akaonekana dikteta lkn miaka kadhaa sasa china iko level moja na marekani, sisi hata kujenga mitaro tunalilia wafadhili, tunahitaji dikteta aina ya watu km mao ze dong.
Kuna watu km wajapani wanafanya kazi kwa masaa 15 kwa siku, sisi masaa sijui nane na nusu tena kwa mbinde kuyatimiza, utakuta mtu analalamika kweli kweli.
Tunasherekea miaka sijui 48 ya uhuru hata barabara tu zimetushinda, kweli tutabaki wadanganyika