YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,001
Japan Ni nchi iliyoendelea Lakini maendeleo Yana gharama kubwa pia.
Mfano mtu akifa Japan kutokana na ukosefu wa ardhi eneo la kuchimba kaburi lazima ununue na linauzwa kwa dola za marekani elfu 40 sawa na shilingi za kitanzania milioni 80 Kama huna maiti ya mtu wako inabidi ichomwe Moto .Kasheshe inakuja majivu ya maiti yako utapeleka wapi sababu pa kuyatupa au kuhifadhi lazima ulipie Sio chini ya milioni nne ukibahatika kupata kampuni ya kuyabeba au dini yao.
NASA wanaorusha vyombo angani wa marekani wamegundua fursa .Kwa dola elfu sita sawa na shilingi milioni 12 wanabeba majivu ya Marehemu mjapan kwenye vyombo vyao vya kwenda anga za juu na kuyatupa huko.Na wanatengeneza hela hasa.Je serikali yetu haiwezi omba tenda ya kubeba majivu na kuja kuyazika Tanzania wakatulipa?
Hii Naona fursa nzuri ya kibiashara.Serikali iangalie Hilo na private sekta pia