Tanzania tufanye nini ili tufanye vizuri kwa mashindano ya kimataifa?

wengi sana wachambuzi washaongea nini cha kufanya lakini TIEFUEFU kichwa cha mwendawazimu
 
Tuwekeze kwenye mambo mengine. Mpira umetushinda.
 
Tuwekeze kwa vitendo kwenye soka la vijana, Tuhakikishe makocha wetu wazawa wanapata mafunzo ya kutosha nje ya nchi, tuajiri walimu walimu wazuri wenye sifa stahili kwenye timu zetu za Taifa, na mwisho kabisa tutenganishe michezo na siasa.

Nb: Mimi si mfuasi wa Amunike! Hata akiondolewa leo,sitamsikitikia kwa lolote maana falsafa zake sijawahi kuzielewa.
 
Uraia pacha kwa wanamichezo. ..unafikiri tungeenda AFCON ..Yondani anasimama na Yakub (Mghana wa Azam) Sita Kingue(Azam..Mcameroon) .nane Tshishimbi (Yanga..DR Congo)..wale wakenya wangetufunga vipi..huu mfano tu..Cape verde walifanya kama hivi wakafanikiwa. ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…