mtumishi mtumishi
New Member
- Jun 22, 2024
- 2
- 1
Ningependa kuwashauri wahusika yafuatayo. Wapanue wigo wa kuwafikia walipakodi kwa kuwa na mipango ya muda mfupi na muda mrefu kwa kufungua ofisi za mamlaka ya mapato kwenye kata na tarafa hata serikali za mitaa ikibidi, kulingana na wingi wa walipakodi kwenye maeneo hayo.
Kodi za ardhi na majengo zikikusanywa kwenye ofisi ndogo za mamlaka ufanisi utaongezeka. Biashara nyingi hazijasajiliwa kwenye mamlaka ya mapato kwani ofisi ziko mbali na walipakodi.
Vipo viwanda vidogovidogo vingi kwenye makazi ya watu na kuna uwezekano hawajasajiliwa na mamlaka za serikali. Hizi ofisi zitakuwa na eneo la kiutawala dogo na wataweza kufuatilia vizuri.
Wafanyakazi wa mamlaka ya mapato wawe na elimu na ujuzi wa kitaalam kuwawezesha kufanya makadirio ya kodi kwa usahihi. Maeneo mengi yana biashara na huduma ni tofauti. Mfano. Wanaokadiria Kodi Kariakoo au Arusha mjini au mijini wawe na shahada ya biashara, au uhasibu, uchumi nk. lakini wa kodi ya majengo awe na shahada ya uhandisi ujenzi, ukadiriaji wa majengo na kama eneo lina ufugaji mwingi awe shahada ya kilimo, mifugo, yaani ile shughuli kubwa ya kiuchumi ya eneo iwe na wataalamu itapunguza sana migogoro.
Uwekezaji mwingi umefanyika kwenye ardhi. Ni vizuri ardhi yote mijini na maeneo mengine yenye shughuli za kiuchumi ipimwe na ijulikane inamilikiwa na nani ili kodi yake ikusanywe. Na ardhi na majengo yakadiriwe kwa ukubwa na dhamani ya soko na kodi yake ikusanywe.
Mamlaka ifanye jitihada kutengeneza mashine za EFD ambazo ni rahisi kutumia na za bei rahisi ili biashara nyingi ziweze kumudu kuzinunua na kuzitumia.
Ikiwezekana serikalini akutane na serikali kama ya china itengenezewe EFD maalumu za Tanzania zenye sifa na mahitaji tuyatakayo kwa biashara na mitaji mbalimbali ya biashara.
Mfumo wa kodi ufanyiwe uchunguzi wa kina kwani watu wengi wanasamehewa kodi kisheria ingawa wana mapato makubwa. Wamo wana siasa na viongozi wengi na taasisi za kidini za kibinafsi.
Ni vizuri huu mzigo wa kulipa kodi ubebwe na kila mtanzania mzalendo mwenye kipato halali na uzalendo uwe pia ni usafi katika kulipa kodi.
Kwa kuwa kodi nyingi zipo kwa asilimia na taasisi za serikali ni nyingi kama EWURA, latra, WCF, mifuko ya hifadhi ya jamii, TRA, TANESCO, (umeme) ukiweka makato haya kwenye gharama za huduma unakuta bidhaa au huduma inakuwa ghali sana na inachochea ukwepaji wa kodi.
Kwa kuwa huduma nyingi zina gharama zingine nyingi kama kodi ya pango, ulinzi, kodi za leseni na za bodi za vibali mbalimbali wale wafanyabishara waaminifu wana hatari kubwa ya kutokukua kibiashara au kufilisika.
Mitambo ya kuhifadhi kumbukumbu za kodi iongezewe ukubwa na ufanisi. Kumbukumbu za kodi kwa mlipakodi kwa sasa ni changamoto.
Unaweza kujua hali ya bima ya gari, lakini mfumo wa kodi bado haupo rafiki kwa walipakodi wetu kuangalia na kusoma faili lake la kodi kama lilivyo kwenye mamlaka. Huu ni mlango mkubwa sana wa rushwa.
Kwa sasa naishia hapa.
Nawasilisha

Upvote
5